Kwanza unatakiwa kuwa na tin namba kutoka TRA na yakulipia sio ya bure, apa utatumia akili kidogo ili wakuchaji pesa kidogo mfano mimi nilienda nikawaambia nimefungua stationary mauzo yangu ni 10000 per day nikawapa nakala ya mkataba wa frem nliopangisha ambayo haikuzid 50,000 kwa mwezi, basi TRA wakanipa form nikaenda kuijaza ikapitia office ya serikali za mtaa nikarudisha nikakadiriwa kodi kama ya 30000 ivi kwa mwaka hatimae nikapewa tin namba ya biashara, next nikaenda halmashauri kufatilia lesen ya biashara, ukienda kwenye halmashaur yako watakwambia nini na nn wanahitaji moja wapo ni iyo tin namba kutoka TRA basi nao ukikamilisha watakufanyia makadirio utalipia baada ya mda kidogo utapewa leseni (ukienda TRA au halmashauri hakikisha umeshajipanga kua biashara gani utaifanya ili kuepuka usumbufu yaan buni ata kwa imagination sio lazima ufungue kwa wakati uo ila vizur zaidi iyo biashara iwe kwenye mipango yako, mfano mm nlibuni tu stationary na saivi nnayo kiukweli lengo la hili ni kupata izo leseni zao tu), ukishapata sasa utaenda office za mitandao unayoka na leseni,tin namba, copy ya kitambulisho, pasport size, kule watakupa form ujaze then watakupa utaratibu mwingine, upande wa voda hawana longo longo wao ni fasta tu na nibure kabisa, ila tigo sasa itategemea na office husika na itachukua mda around 2-5 month. Uo mtiririko kiutendaji ni simple sana ukiwa upo fresh haumalizi ata siku 3, mfano mimi TRA nilimalizana nao kwa siku moja tu.
Ushauri usijaribu kabisa kutumia doc au line iliosajiliwa na mtu mwingine, wakati wa kutumia inakua haina tatizo ila likitokea tatizo lolote ukahitaj msaada wa moja kwa moja kutoka office za mtandao husika utahitajika docmnt zote za usajili na lazima taarifa za iyo line zipelekwe na mhusika nakwambia hivi nikiwa na uzoefu wa kutosha.