Msaada: Kwa nini scania na sio volvo?

Hao ndo Wabongo tulivyo! Wachina wanatujua vema kulivyo tunavyojijua. Wachina wanachakachua tu bidhaa za makampuni yenye majina makubwa tu mfano..nokia, sony, hitachi, LG, samsung nk.. Ni ugonjwa unaohitaji tiba ya muda mrefu. Ni maoni yangu binafsi japo si mdau wa usafirishaji.
 
Bobby, hapana si beleaf ni hali halisi ya biashara ilivyo. Hata ukienda kukopa kwenye haya mabenki yenye uzoefu wanakuwa na imamni kubwa kumkopesha anaenunua Scania kuliko magari mengine ambayo hayajazoeleka hapa nchini. Hata ukifanya utafiti mdogo wanalipa madeni wengi ni wale wanakopa kununua magari ya Scania. ni ukweli usiopingika kwamba kweli Scania ni ghali kuwekeza lakini resale value iko juu sana. Mfano ukinunua Scania kwa ml 60 baada ya miaka mitano kama unalitunza vizuri utajaliuza kwa ml 40-50! Mungu akupe nini. Taarifa zilizoko ni kwamba Scania Tanzania wana asili mia 80 ya vipuri unavyohitaji! Kwa hivyo uwakilishi wake unaendana na wakakti. Nawasilisha.
 

Mkuu Chesea Ingine, kwanini hayo mabenki unayaondoa kwenye hiyo "belief"?. Wao ni sehemu ya soko na wapo kuwahudumia wateja ambao imani yao ni scania trucks tu na si vinginevyo. Unajua wanaodetermine hali ya sokoni ni wateja na wauzaji (demand & supply) na si vinginevyo kwa hiyo effect ya hiyo hali inacut across kote mkuu including kwenye mabenki. Unasema wanaolipa mikopo wengi ni wale wenye scania huenda sababu ni kuwa wanaonunua scania kwa mkopo ni wengi kuliko wa volvo. Mimi ninahitaji opinion ya kiufundi kwamba Scania ni bora kuliko Scania otherwise kilichopo hapa ni imani na may be ni ulimbukeni tu kama mchangiaji mmoja alivyosema.Nchi zote zilizotuzunguka watu wa scania wana ofisi huko pia lakini hawana scania nyingi kama tulizo nazo sisi. Sitaki kuamini kwamba sisi tunajua kipi kilicho bora kuliko majirani zetu wote.Kuna jamaa wachache ninawafahamu ambao wanajuta kwanini wamepoteza muda wao mwingi kwenye scania bila sababu ya msingi.
 
Mkuu,
Hayo ndiyo maneno.Kutokana na wingi wa Scania na baada ya kumshawishi mtu anayefanya biashara ya transportation anunue Volvo akakataa kama nilivyo mention hapo juu ni kaanza kuwa na wasi wasi labda kuna matatizo ya kiufundi. Nikamwuliza fundi mmoja nje ya nchi anaye deal na Scania na Volvo akaniambia hajaona tatizo lolote.Lakini bado kiasi fulani nikawa na wasi wasi ndio nikaamua kuja hapa HOME OF GREAT THINKERS, so far kutokana na majibu niliyoyapa hasa kutoka kwako wasi wasi wangu umeisha.Nilichojifunza hapa mpaka sasa hivi Watanzania wengi ambao ni wafanyabiashara hawataki kutoka out of their comfort zones.
 
Muelewe kuwa hizi zote ni Swedish companies na kupunguza ushindani wanaweza kuwa walifanya market seggregation...Scania ije Tanzania na Volvo iende kwingineko....ni kama ilipo VODACOM na MTN haitii mguu.....nakubali kuwa Volvo inaweza kuwa na ubora lakini bado Scania ina mengi mazuri kuliko Volvo kama utumiaji wa mafuta
 
...........nimekukubali camaraderie,...........kwa kuunga hoja mkono,tetea kitengo naona umechangamka na tayari uko stand by kwa kupokea order...........duh mchaga utamjua tuuuuuuuuuuu,............................
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…