Wanasayansi wanasema huko anga za juu kuna galaxy trillion mbili na kila galaxy ina nyota 200 billion
Taarifa hii si ya kweli.
Kulingana na wanaanga,
hakuna taarifa yenye idadi kamili ya Galaxy 🌌 na idadi za nyota iliyo fixed.
Huwa ni makadirio tu.
Kuna Galaxy kubwa kama hii yetu (Milkway), kuna Andromeda n. K
Galaxy ya Andromeda iliyojirani kabisa na Milkway inakadiriwa kufikisha nyota trillion 1,
Milkway yenyewe inakadiriwa kufikisha nyota billion 100
Kuna dwarf galaxes nyingi tu ambazo hazifikishi hata nyota billion.
Zipo zenye makadirio ya nyota 1000 makumi elfu na kuendelea hadi billion
Mojawapo ya dwarf galaxes zilizokaribu zaidi na jua letu ni
Canis Major Dwarf Galaxy iko umbali wa kilometer 236,000,000,000,000,000, sawa na miaka ya mwanga 25,000 kutoka kwenye jua.
Sagittarius Dwarf Elliptical Galaxy inafuata iko umbali wa Kilometer 662,000,000,000,000,000 sawa na miaka ya mwanga 70,000 kutoka kwenye jua letu.
Hivyo ni bora zaidi kuchukua taarifa kama zinavyotolewa na source husika.
Cha ajabu wanasema nyota moja ni kubwa Kuliko dunia yetu.
Nyota moja? Hii taarifa unaitoa wapi?
Unaweza kulinganisha nyota yeyote na dunia kwa ukubwa?
Dunia ni kitu kidogo sana kwenye space.
Nyota ni madude makubwa sana japo yanatofautiana size, lakini kulinganisha nyota yeyote ile na sayari ni kichekesho
Je ukubwa wa anga ukoje? Ukubwa wa anga ukoje Hadi ukabeba vitu vyote hivyo
Hadi sasa naweza sema hakuna ukomo wa anga, ulimwengu unaendelea kutanuka kila kukicha.
Ukitizama utaona jinsi vitu hivi vinavyoendelea kutengana!/kukimbiana
Kama anga imebeba vitu vyote hivyo basi salute kwa Mungu.
Mungu yupi unayemuongelea hapo?
Habari ya Mungu/miungu haiwezi/haziwezi kuthibitishwa kisayansi.
Hapo unaenda kwenye kuamini siyo ujuzi uliotaka tuujadili hapa.
Je unataka kujua au kuamini?