Kiungonguli
Member
- Jul 26, 2015
- 60
- 100
Arusha. “Ninaomba kama kuna mtu anajua dawa ya hawa watoto kuacha kula magodoro anisaidie, maana hadi mimi mwenyewe naogopa, natamani hata kukimbia hii nyumba,”
Hiyo ni kauli ya Joyce Mrema (45), mama wa watoto pacha wa kike, mkazi wa Mtaa wa Kanisani uliopo Kata ya Sokoni One jijini Arusha ambaye watoto wake wana changamoto ya kula madogoro kwa muda wa miaka sita sasa.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi nyumbani kwake mwishoni mwa wiki, anasema aligundua watoto wake wana tabia ya kula magodoro walipokuwa na umri wa miaka mitatu na kueleza awali alidhani ni utani au michezo ya watoto, lakini baadaye hali hiyo iliendelea mpaka sasa.
Anasema watoto hao wenye umri wa miaka tisa sasa wapo darasa la nne na kutokana na changamoto hiyo wanashindwa kufanya vizuri darasani.
Joyce anasema analea watoto hao mwenyewe kuanzia mwaka 2013 baada ya baba yao kuondoka, wakati huo watoto wakiwa na umri wa mwaka mmoja na miezi mitatu na hadi sasa hajui alipo.
“Niligundua watoto wangu wanakula magodoro walipofikisha umri wa miaka mitatu. Mwanzo nilikuwa nawachapa kwa sababu nilijua wanachezea. Wanakula wanameza, chakula hawali, wanatupa chooni.
“Ukiwapa kikombe cha maziwa, ukitoka nje ukirudi unakuta mtoto anatoka chooni na kikombe cha maziwa, unakuta maziwa amemwaga chooni,” anasema na kuongeza:
“Mara nyingine nikiwapa chakula wanatapika. Kuna walikuwa wanaumwa matumbo na wakiharisha unaona vpande vya magodoro.”
Anasema baada ya kubaini hali hiyo, aliwapeleka kituo cha afya Levolosi ambako nesi alimweleza watoto wake watakuwa na upungufu wa madini, hivyo akamtaka awape dagaa na cauliflower. Hata hivyo, anasema alipowapatia vyakula hivyo, hali haikubadilika.
Joyce anasema ilifika wakati alishonea kava kwenye magodoro kwa lengo la kuwazuia wasile, lakini waliendelea kula na kwamba walifikia hatua ya kwenda kula magodoro yaliyokuwa kwenye mito ya kulalia na sofa za wapangaji katika nyumba wanayoishi.
Anasema kutokana na changamoto hiyo, baadhi ya wapangaji walihama huku naye akishindwa kwenda kujishughulisha na kazi za kujiingizia kipato, ili apate muda wa kukaa na watoto hao na kuwazuia wasile magodoro.
“Kwa sasa shughuli inayoniingizia kipato mbali na kupangisha vyumba vichache vilivyopo katika nyumba hii, ni kufua nguo za watu. Nalipwa kuanzia Sh 3,000, sichagui kazi.”
Kuhusu chakula wanachopenda, mama huyo anasema hawapendi chakula chochote na anapowalazimisha mara nyingi huugua tumbo na kutapika.
“Wakati mwingine wakila chakula wanadai tumbo linawasokota, lakini wakati mwingine nikiwapa uji au maziwa hawatapiki. Ukisikia wanasema tumbo linasokota ujue wamekula magodoro.
“Ningekuwa na uwezo ningeenda hospitali nyingine kubwa, imefika hatua nalazimika kuweka pilipili kwenye masofa labda wakinyofoa watawashwa, ili waache kula lakini bado,” anasema mama huyo.
Joyce anasema changamoto hiyo imesababisha watoto wake kutopenda kusoma, hali inayosababisha wafanye vibaya darasani huku akilalamika baadhi ya majirani zake wamekuwa wakimtolea maneno ya kashfa dhidi ya watoto wake.
Kuhusu mume wake, anasema tangu alivyoondoka mwaka 2013 hajarudi na sasa ana kesi iliyosababishwa na mkopo wa Sh3.5 milioni ambazo mume wake aliuchukua bila kumshirikisha na sasa anadaiwa zaidi ya Sh30 milioni.
Anasema kesi ya madai hayo inaendelea baada ya kukata rufaa, kwani alitakiwa kuondoka kwenye nyumba wanayoishi ambayo iliwekwa rehani na mumewe alipokuwa amekopa fedha hizo.
Watoto waeleza
Wakizungumza na Mwananchi, watoto hao wanasema licha ya kutamani kula chakula, lakini hawawezi na badala yake wanapata hamu ya kula magodoro. “Sijui kwa nini nakula magodoro, lakini nasikia hamu ya kuyala tu, napenda wali maharage lakini nashindwa kula,” anasema Dotto.
Kulwa anasema: “Najisikia tu hamu ya kula magodoro, lakini sipendi kula chakula na mama akiwa nje mimi nakula magodoro ndani.”
Mwanasaikolojia afunguka
Mtaalamu wa saikolojia, kitengo cha afya ya akili kutoka Hospitali ya Rufaa ya Mount Meru, Emanuel William anasema watoto hao wana tatizo la kisaikolojia kitaalamu linalitwa ‘Pica’.
Anasema tatizo hilo lipo kwenye changamoto ya kula (eating disorder) ambalo humsababishia mtu kula vitu visivyo na virutubisho.
Anasema mara nyingi hali hiyo hutokea kwa watoto na wajawazito. Mjamzito hupata changamoto hiyo anapokuwa na upungufu wa madini ya zinki au chuma inayomsababishia kula vitu kama udongo na mkaa.
“Kwa watoto ni tabia ambayo si ya kawaida, mtoto akiwa na tabia, tatizo halizidi wiki mbili hadi mwezi, vinginevyo inakuwa changamoto ya kisaikolojia au afya ya akili kwa hiyo mtoto anahitajika apate msaada,” anasema.
“Mara nyingi hii shida huwa kwa watoto wenye ulemavu wa akili. Mfano ambaye hana uwezo mzuri darasani au ana shida ya kuelewa au kuandika, kujua masomo asilimia kubwa hupata shida ya kula vitu ambavyo si vya kula.
“Hii shida mara nyingi huwa kwa wale wenye dalili ya ugonjwa wa afya ya akili kwa mfano hali ya kuchanganyikiwa,” anasema.
Anasema matibabu ya changamoto hiyo huanza kwa kuzungumza na mzazi kujua historia yake tangu alipokuwa mjamzito, alipojifungua, ili kufahamu chanzo cha tatizo hilo.
Anasema kuna masuala ya kibaiolojia na kulingana na namna mama alivyokuwa mjamzito kama alikuwa na tabia ya ulevi, hakuzingatia kliniki au alipitia changamoto za kijamii zinaweza kusababisha mtoto au watoto kuwa na tatizo la kisaikolojia.
Mtaalamu huyo anasema hali kama hiyo ikitokea kuna matibabu ya aina mbili---ya kisaikolojia na matibabu ya dawa na kwenye dawa lazima daktari atawapima watoto kwanza ajue wameathirika vipi kimwili na pia kuna upungufu gani ili wapatiwe dawa.
Kwenye tiba ya kisaikolojia anasema watakaa na watoto kuwaangalia tabia zilizopo na kujua imewaathiri vipi. “Tiba ipo, hili tatizo si la kishirikina, ni tatizo ambalo lipo kwenye mambo ya afya ya akili,” anasema.
Anasema watoto hao wanaweza kupatiwa tiba na baada ya tiba tatizo halitajirudia, ila tiba yake huwa ni endelevu.
““Baadhi ya watoto wamekuwa wakila udongo, mkaa, chaki au karatasi, lakini hii ya magodoro imekuwa ya tofauti, inashangaza hata mimi nilipoona ikanishangaza nikatamani kujua ili nione shida iko wapi.”