Msaada; kwa yeyote mwenye uzoefu na nissan x-trail

mpungara

Member
Joined
Nov 16, 2011
Posts
75
Reaction score
17
Ndugu zangu nataka kununua Nissan x-trail ila sina uzoefu na gari hizi, naomba mwenye uzoefu nazo anipe ABC zake, je nini matatizo makubwa hasa ya gari hizi? consumption yake ya mafuta ikoje?
 
Usinunue yenye trubo.otherwise ni gari tamu kwa kweli.ukiwa na safari ya mbali ndiyo utaipenda zaidi
consumption iko reasonable.spares ziko kibao ilala.bei kawaida kabisa.
 
yale toleo la mwanzo stability mbovu sana labda upate new model wameyachora vizuri ile model ya mwanzo ukilala nayo kwenye kona hata na 60 inaweza kukuua
 
We nae unataka kununua gari gani kiongozi!!!
Itakusumbua achana nayo.
 
Ndugu zangu nataka kununua Nissan x-trail ila sina uzoefu na gari hizi, naomba mwenye uzoefu nazo anipe ABC zake, je nini matatizo makubwa hasa ya gari hizi? consumption yake ya mafuta ikoje?
Ni ya kike
 
Usinunue yenye trubo.otherwise ni gari tamu kwa kweli.ukiwa na safari ya mbali ndiyo utaipenda zaidi
consumption iko reasonable.spares ziko kibao ilala.bei kawaida kabisa.
Msiwe mnakariri amekwambia yuko tz ???
 
Habari wana Jf, natumai mu wazima. Leo naomba kuuliza wataalam walio wahi kumiliki/Kutengeneza gari aina ya Honda Fit, naomba kujua yafuatayo:
1. Ustahimilovu wa miundombinu (Barabara za Tanzania).
2. Ulaji wa mafuta (Compared to IST, VITZ, RAUM-JAMII YA TOYOTA)
3. Upatikanaji wa spare zake na gharama za spea.
4. Kwanini sio nyingi mjini.
5. Je inafaa kufanyia biashara ya UBER??
Asante, naomba kuwasilisha.
 
Ndugu zangu nataka kununua Nissan x-trail ila sina uzoefu na gari hizi, naomba mwenye uzoefu nazo anipe ABC zake, je nini matatizo makubwa hasa ya gari hizi? consumption yake ya mafuta ikoje?
Salaam,

Unahitaji kujua kuhusu Nissan x-trail ya mwaka gani.?!

As a car dealer, ushaur wangu naweza kukupa kulingana na mwaka husika wa gari sababu hua zinatofautiana sifa kukingana na mwaka.
 
yale toleo la mwanzo stability mbovu sana labda upate new model wameyachora vizuri ile model ya mwanzo ukilala nayo kwenye kona hata na 60 inaweza kukuua
Cjawai ckia accident ya gar aina ya xtrail hpa bongo. Alteza ndzo znaongoza kwa vifo
 
Salaam,

Unahitaji kujua kuhusu Nissan x-trail ya mwaka gani.?!

As a car dealer, ushaur wangu naweza kukupa kulingana na mwaka husika wa gari sababu hua zinatofautiana sifa kukingana na mwaka.
2001 ikoje mkuu?
 
Hakuna ajali inayosabaishwa na gari, ajali zinatokana na uzembe wa dereva/muhusika. Hakikisha gari yako ipo good condition muda wote na uendeshaji wa sheria na tahadhari, hutakaa usikie ajali kwako.
 
Back
Top Bottom