Msaada kwanini natetemeka sana?



Huko ndio ntakufa kabla maana nikijitahidi kulazimisha kuongea jasho linanitoka hata kama kuna baridi na mikono saa hio haiwezi kishika kitu!!
 

Punguza pombe
 
Last edited by a moderator:

Nadhani ww utakuwa engineer au mwanasayansi maana ndiyo huwa hawajiamini wakiongea mbele za watu
 
Last edited by a moderator:
Hata ninaposoma hizi post nnakua na hofu utadhani watu wananiona

Duh!! Kweli una tatizo....yani hata ukisoma pia hali ni hiyo? Itabidi uonane na watu wa saikolojia wakusaidie lkn maombi pia ni muhimu
 
hili tatizo hata mi lilinisumbua sana
 
Mimi ni mnywaji sio mlevi

mkuu hilo tatizo linatibika onana na psychologist ungekuwa dsm ungeenda muhimbili session chache tu umepona...

afu pia mkuu you need to orient youself close to people, practise kuongea nao mambo mbali mbali.

anza na marafiki zako wakaribu alafu jichanganye kwenye group za watu hakikisha unaongea mkuu, wewe ni unique hakuna kama ww so jiamini..

asikudanganye mkuu kila mtu hua ana hofu akianza kuongea mbele ya mkusanyiko mwingi wa watu lakini zinatofautiana zile first minutes za kutolarate huo uwogo!!

jiamini jembe ndo key yakutokuogopa!!...afu pia piga prayer sana arif
 

Asante sana arifu!!!
 

Kumbe tupo wengi. Hata mimi nina tatizo hili. Nimekuwa nalo tangu nikiwa shule ya msingi. Nilikuwa bright darasani, lakini ilipokuwa ikifika mwalimu akaninyanyua nisome hata aya moja kwenye kitabu cha kiswahili nilikuwa nashindwa kabisa. Siku moja alikuja mwalimu wa kiswahili mgeni--alihamia shuleni kwetu--akaniambia nisome (tulikuwa tukisoma kwa zamu--kwa wale wanafunzi mliosoma miaka ya 80's mnafhamu hili). Nilishindwa kabisa. Basi siku hiyo aliporejea Staff room, akawauliza walimu inakuwaje mwanafunzi wa drs la sita asijue kusoma. Wakamuambia mimi ndiye genius darasani ila hiyo habari ya kusoma vitabu darasani siiwezi kabisa. Bado hali hiyo ninayo mpaka leo. Kujieleza mbele ya kikundi cha watu 5 au 6 ni shida sana, hasa pale ninapokuwa nimechukua nafasi ya main speaker huku watu wote wakinitazama na kunisikiliza--points zote nilizokuwa nataka kuongea huyeyuka na kijasho jembamba huanza kunitoka.
 


Mi sipendi kabisa nikiongea mtu aniangalie machoni yaani basi tu !!"""
 
Pole Apolinary...ila kuna psychologists wengi wanaweza kukusaidia ,labda ufanye utafiti mwenyewe kwenye mtandao utapata nafuu....namfahamu mhindi flani kazini ambaye pia hutetemeka tu kila mara anapo anza kuzungumza.
 
Pole Apolinary...ila kuna psychologists wengi wanaweza kukusaidia ,labda ufanye utafiti mwenyewe kwenye mtandao utapata nafuu....namfahamu mhindi flani kazini ambaye pia hutetemeka tu kila mara anapo anza kuzungumza.


Alafu hii hali hainiruhusu kujichanganya na wengine naona nitajichanganya!

Amani Usalama hakuna!!!
 
vip mkuu ulifanikiwa kuwaona wanasaikolojia?
 
Alafu hii hali hainiruhusu kujichanganya na wengine naona nitajichanganya!

Amani Usalama hakuna!!!

Hali kama yako ilinikosesha kazi sehemu nyingi sana, nikiingia kwenye interview nilikua natetemeka nusu kufa.. jamaa wakiangalia vyeti nilivopasua wanashangaa ile mbaya
nikaanza kwenda shule flani flani nawafundisha watoto..
kwa sasa naweza kuhutubia hata watu 500 bila kuogopa.. pia ni muongeaji mzuri..nimekua kiongozi sehemu mbalimbali.. ndugu utakosa fulsa.. jitutumue.. tatizo ni kulelewa na wazazi wababe.. mimi baba yangu alikua mtu wa ajabu sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…