Msaada kwenye kiwanja

Msaada kwenye kiwanja

Chacha wa marwa

Senior Member
Joined
Jul 5, 2013
Posts
116
Reaction score
20
Kuna kiwanja kimeingiliana na jirani yangu, ambapo kwenye hicho kuna nyumba yangu na ya kwake, sasa kwakuwa nyumba yake ni kubwa inavyumba 8 anataka achukue hati ya hicho kiwanja nyumba yangu ina vyumba 3 je sheria inasemaje? Naomba msaada wenu wana jamvi maana naona kama nataka dhurumiwa.
 
Ni vizuri ukatuambia kwanza mazingira ya upatikanaji wa kiwanja husika. Ilikuwaje mpaka wote mkajenga kwenye plot moja?
 
Ni vizuri ukatuambia kwanza mazingira ya upatikanaji wa kiwanja husika. Ilikuwaje mpaka wote mkajenga kwenye plot moja?

Asante ngoja nikupe jinsi ilivyo, nilikuwa na eneo mnamo mwaka 90 niliuza kipande kidogo,wakati huo walikuwa hawajapima viwanja,walipo kuja kupima vikatoka viwanja 4,ukitoa kile kipande nilichouza vinabaki vyangu 3na nusu, ile nusu alikuwa amejenga nami pia kulikuwa na nyumba, ndo yeye anahitaji kuchuku hati ya kumiliki anadai kuwa nyumba yake ni kubwa, sasa kuhusu hiyo nyumba yangu na hiyo nusu uwanja sheria inasemaje naomba msaada.
 
kwa kesi kama hiyo, nataka kufahamu kama mlijenga baada ya kupimiwa hivyo viwanja au la. Na pia wakati wanapima viwanja wapimaji waliona kuwa kuna plot ina nyumba mbili na wao wakapima vivyo hivyo hivyo kuwaacha ndani ya plot moja ? Kama mlijenga baada ya eneo kuwa limepimwa nani alipewa kibali kisheria kuwa mmiliki wa eneo mnalogombania au wote mmevamia na kuanza ujengi bila kushirikisha vyombo husika?
 
Back
Top Bottom