Msaada kwenye majibu ya utrasound report

Angekuwa na dalili ya Polycystic Ovarian Syndrome malalamiko yake yangekuwa tofauti kabisa, umeshawahi kukutana na mgonjwa wa Polycystic Ovarian Syndrome au theory tu?

 
Ningemshauri mleta hoja akuone umfanyie hiyo sornography afu kama ataridhia utupe findings..maana naona miluzi mingi humpoteza mbwa...
 
Kinachonifuraisha JF bana topic ikiwa ya Maloveee asee hapa kurasa nyingi zingeshajazwa, lakini jambo kama hili linapigwa danadana tu! Hivi kweli humu JF hatunaga madaktari wa ukweli jamani. Hebu madaktari mjitokezee!
Natamani kwenda kusomea udaktari-pamoja na kupewa 100% ya mkopo mavyuoni bado hollaaaaa!
Bora serikali iwaruhusu "lambalamba" basi!:A S 39:
 
Angekuwa na dalili ya Polycystic Ovarian Syndrome malalamiko yake yangekuwa tofauti kabisa, umeshawahi kukutana na mgonjwa wa Polycystic Ovarian Syndrome au theory tu?
Mkuu Kop hiyo nimekujibu

wewe uliye niuliza kuhusu Hormone sikumjibu aliye uliza swali jaribu kunielewa vizuri usichanganye mambo tafadhali

ninarudia tena hatukuja hapa kushindana mimi na wewe tumekuja hapa kumsaidia mwenzetu wewe toa ushauri wako

na mimi ninatoa ushauri wangu jibu nimesha mjibu aende hospitali ingine kuangalia vizuri na pia ikiwezekana aangalie

Hormone birth zake zikoje? wewe usilete mambo ya Ligi hapa tafadhali hatukuja kushindana kama unaweza msaidie huwezi achana nae ndio hivyo usinikwaze mimi.Naona unataka kuniharibia siku yangu ya leo Mkuu Kop niache kama nilivyo samahani.
 
Si ndo maana nikashangaa dr asiejua multiple follicles ni wa wapi? Uvivu nayo! Anashindwa hata kugoogle jamani?
Unajua nikiangaliaga medical mysteries documentaries za wenzetu na jinsi wanavyo dig put na kutatua tatizo; huwa najiambia huku kwetu tunachoita kulogwa ama kutotibika ni uvivu tu wa kufikiri wa madaktari japo unachangiwa na hali ngumu ya mazingira ya kazi na kukosa vifaa. Nilikutana na clinical officer mmoja akaniambia tetanus inasababishwa na kutu ya kwenye msumari (nilikuwa na kidonda nikataka kupata sindano za antitetanus). Nilijichokea nikaenda hosp nyingine.
 
Samahani sana kama naelekea kuharibu siku yako, hata mimi ligi sitaki. Let me declare professional interest, am a Doctor and I know what am doing.
HORMONE BIRTH ndio nini ?????
Ukimwambia mgonjwa apime hormone lazima uwe specific apime hormone gani...!!!
Ni hayo tu mkuu, nisamehe kama siku yako itaisha vibaya. Lakini madaktari lazima wachimbane mgonjwa afaidike
 

acha dharau unaweza kuwa md ila mweupe sawa na huyo co or amo
 
hata mimi nakuunga mkono...

majibu ya daktari utayajua tu hata kama hukusomea udaktari.Muwe mnakuja mara kwa mara wakuu kuondoa upotoshaji hapa.Majibu ya Zemarcopolo kwa mfano,yanaonyesha kabisa ni daktari na siyo mtu wa copy paste
 
Reactions: Kop
Tembelea hapa kuijuwa hiyo hormonal birth control. http://www.acog.org/~/media/For Patients/faq159.pdf?dmc=1&ts=20130325T1444394436
 

umekuja kujifunza humu au?

ukisoma post ya mdau utaona kuwa mawasiliano na mwenzio yanaendelea na wala sio ktk hii thread walipoanzia.

kama unataka kuwa mshauri kama mzizi basi weye komenti ishia mtu akisoma ataona utofauti na kuchagua wafate ushauri wako au wake.

sio kukosoa kosoaaaaaaaa tu, WEKA POINT ZAKO AU USHAURI MAMBO YASONGE MBELE

mmhh kudandia
 
hakuna mtu anayekosolewa..wala hakuna foolish questions but inadequate answers, dhumuni la kuuliza ni kuelewa, hakuna mwisho wa kujifunza kila siku tunajifunza
 
Nchi za Ulaya kuna utaratibu kwamba ultrasound za gynecology zinafanywa na gynecologist na yeye mwenyewe ndiye anayemueleza mgonjwa ameona nini na kinamaanisha nini.

Kwa kwetu Tanzania kwa vile specialists ni wachache basi ni vema kukawa na utaratibu yule aliyepiga ultrasound awe anawajibika kumfafanulia mgonjwa majibu aliyoona.

Katika case hii kama sonographer ameziita follicles basi hazina tatizo. Kwa sababu hizo wanawake wote walio kwenye umri wa kuzaa wanatakiwa kuwa nazo. Kukishakuwa na tatizo sonographer anawajibika kuelezea zaidi characteristics za hilo tatizo kama vile ukubwa, contents zake (echogenity), blood supply, uhusiano wako na organs zingine etc.

Hata hivyo kwa sababu hili tatizo lina historia yake ambayo kaka yangu MziziMkavu anaijua na sisi wengine hatuijui, basi ushauri wake unakuwa na thamani ya ziada kutokana na kuwa na taarifa zaidi (information is power)...
 
Last edited by a moderator:
Mkuu ZeMarcopolo Ni kweli ulivyo jibu huko kwetu hakuna vifaa vingi kuliko huku nje ulaya kuna vifaa vingi lakini Ma-Daktari wenye ujuzi ni wachache. Tofauti na nyumbani kuna kuna Ma-Daktari wanao ujuzi lakini Vifaa vya kufanyia Uchunguzi wa Mgonjwa ndio shida kupatikana Mimi ninafikiri Hapo Tanzania kungelikuwepo na vifaa vya uhakika vya uchuınguzi Wagonjwa wasingelikuwa wanapelekwa Eti India au south Africa kwenda kutibiwa. Waswahili Wamesema Kwenye Miti hakuna Wajenzi.
 
Kwa mtazamo wngu hapa Madam G ndo kapotezwa kabisaaa....kwa sababu wenye ujuzi wenyewe wanagongana sasa mgonjwa si ndo hofu inazidi!

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Ni hospitali ya Aghakan Iringa
 
alienifanyia utra sound alisema haoni tatizo nipeleke majibu kwa daktari
 
Kwa mtazamo wngu hapa Madam G ndo kapotezwa kabisaaa....kwa sababu wenye ujuzi wenyewe wanagongana sasa mgonjwa si ndo hofu inazidi!

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
Usiogope mkuu wote majibu yao nayasoma alafu nayatafakari hakuna hata mmoja ambaye ananitakia baya so wote majibu yao ntayafanyia kazi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…