Huwezi kuamini, historia siku zote hujirudia. Huyo mdada amekuumiza hivyo wakati mkiwa wachumba, atakuumiza tena ikiwa hatimaye utamuoa. Hilo uwe na uhakika nalo. Ikiwa anakupenda kweli wala asingekuonesha madharau kiasi alichofanya. Kukurudia ni kuwa sasa anaona huko aliko kuwa amepata amemwagwa. Kama unakubali kuwa spare tyre, yaani namba wani yake ikifeli anarudi kwako, kubali, ila ujue utaumizwa tena.
Mapenzi siyo kitu permanent. Huja na kupita. Uaminifu na heshima huwa ni tabia, hivyo havibadiliki. Sasa kuna kujidanganya kuwa unampenda, au yeye akudanganye kuwa anakupenda. Ikiwa hana heshima na si mwaminifu kama alivokwishathibitisha, kumuoa itakuwa balaa zaidi. Kilele cha mapenzi huwa kipo wakati wa uchumba. Mkishaoana mapenzi huaza kupungua kadri siku zinavyoendelea. Sasa fikiria mtu anayefanya hayo wakati wa kilele, atafanyaje mapenzi yatakapoisha?
Tulioko kwenye ndoa tunajua kuwa miaka mitano down the road, huwa mapenzi hakuna tena. Kinachobaki ni kuheshimiana na kuaminiana tuu. Yaani ile commitment ya viapo vya ndoa inabaki ni muhimu zaidi kuliko mapenzi yenyewe. Kwa hali hiyo umeshajua kuwa huyo mpenzi wako hakuheshimu. Ila circumstance tuu ndo inamrudisha kwako. Utakuwa umefanya kosa kubwa kuusikiliza moyo unaokuambia eti unampenda. Ndoa zoote watu huanza wakisema tunapendana. Lakini mkiisha ingia ndani ya ndoa, other qualities, huwa muhimu kuliko mapenzi pekee.
Be careful, mapenzi yanaweza kukuingiza kwenye balaa wakati unaliona. Hata kama unampenda, achana naye. Tafuta mwingine. Huyo ameshathibitisha kitu kimoja kwako. Si mwaminifu, hakuheshimu, ukimng'ang'ania umeliwa au imekula kwako!!!