Msaada kwenye uandishi wa kiswahili

Msaada kwenye uandishi wa kiswahili

hidencode

Member
Joined
Nov 8, 2018
Posts
13
Reaction score
9
Naomba watalaamu wa kiswahili wanisaidie kwanini tunaandika Mbwa badala ya Mmbwa,Mbu badala ya Mmbu na ikizingatiwa kimatamshi tunatamka Mmbwa na Mmbu badala ya Mbwa, Mbu?

Maneno yapo mengi ila hayo ni kama mfano
 
Kuna udondoshaji hapo, kuna vitamkwa vinaondolewa ili kuboresha lakini udondoshaji wa vitamkwa unatakiwa usiathiri maana. Katika neno umbwa tuna dondosha u na kupata mbwa
Mifano mingine ya udondoshaji

Mujomba --- u-- mjomba

Mutu --u--- mtu

Inge ---i--- nge

Muzinga---- u---- mzinga

Baada ya mifano hiyo Fanya zoezi lifuatalo

Dondosha vitamkwa katika Maneno yafuatayo

Muti

Lifuti

Mutoto

Inzi

Muvua

Muvuvi

*Karibuni wengine kwa mawazo
 
Naomba watalaamu wa kiswahili wanisaidie kwanini tunaandika Mbwa badala ya Mmbwa,Mbu badala ya Mmbu na ikizingatiwa kimatamshi tunatamka Mmbwa na Mmbu badala ya Mbwa, Mbu?

Maneno yapo mengi ila hayo ni kama mfano
Nimesha kujibu hilo lakini kukuongezea maarifa kuna uyeyushaji pia. Kuna maneno huwa yanaugumu kidogo wakati wa kutamkwa hivyo kitamkwa u huwa w ili kurahisisha uzungumzaji.
Mfano

Mualimu -- Mwalimu

Muembe ---- mwembe

Muizi --- mwizi

Muimbaji------ mwimbaji

*Karibuni wadau wengine kwa msaada zaidi
 
Shukrani mkuu kwa majibu yako
 
Back
Top Bottom