Habari zenu wana urembo,
Naomba msaada wa kupewa ushauri wa moisturizer gani nzuri kuupaka usoni kwa wale wenye combination skin or oily skin uso wangu una mafuta ambayo hayachemki bali yanaganda na kutoa weupeweupe flani hivi usoni.
Sio siri unaninyima raha rangi ya ngozi yangu ni brown naomba katika ushauri huo mnisaidie mositurizer ambayo itanifanya ngozi yangu ibaki hivyo hivyo brown coz sipendi kujichubua kabisa.
Watu wenye mafuta mengi usoni nawashauri waanze kwa kuyapunguza mafuta kwanza kabla ya kuhangaika na vipodozi vingine kama lotion na cream.
Kuna poda zinaitwa POND'S (Oil Control Talc) hizi husaidia sana kupunguza mafuta na kufanya ngozi ya mtu kuwa ya kawaida na inayokubali vipodozi vingi zaidi. Poda hii ni nafuu sana (Sh 3,000/= - 3,500/=) na hupatikana kwa urahisi kwenye maduka mbalimbali ya vipodozi, cha msingi iwe original na iwe OIL CONTROL TALC.
Sambamba na poda hizo kuna sabuni za PEARLS ambazo ni mahususi kabisa kwa ajili ya kupunguza mafuta.
Pia nawashauri mtumie FACE WASH/CLEANSER, husaidia kuondoa uchafu unaoziba matundu ya kutokea jasho na mafuta.
Epuka scrub, hususan kama haupaki mafuta. Maana baada ya hapo mwili utazalisha mafuta mengi zaidi.
Kwenye uchaguzi wa lotion nashauri tafuta lotion ambazo zimeshauriwa na kuandikwa FOR OILY SKIN.
Kwa ushauri zaidi na huduma za urembo na vipodozi basi mnaweza mkakaribia kwenye ukurasa wa facebook uitwao S&E BEAUTY SOLUTIONS na kuLIKE ukurasa huo kwa habari na mafunzo zaidi.
Mawasiliano : 0 659 528 724 na 0 784 082 847
Nawatakia kila la kheri katika kujipodoa na kupendeza!