Msaada lugha ya alama

Msaada lugha ya alama

1gb

JF-Expert Member
Joined
Jun 30, 2013
Posts
2,199
Reaction score
2,859
Wana jf.

Juzi nimetembelewa na mtoto wa dada angu,sasa huyu mjomba ni bubu,sasa kwa siku mbili hizi nilizoo kaa nae,yaani hatari. Kwanza anaonekana mwongeaji sana (kwa lugha za Alama).

Pili ni ananipenda sana muda woote yupo karibu na mimi labda kutokan na nilivyoondoka alikuwa mdogo sana. Sasa kasheshe linakuja kwenye mawasiliano. Mara akunje ngumi,mara aonyeshe vidole vitatu,mara viwili kama chama flani hapa TZ.Mara ashike kidevu japo hili nafahamu kuwa ni jinsia ya kiume.

Sasa amenifanya niwe nachelewa kurudi nyumbani,kwa kuhofia nikifika sitting room ataanza mwembwe zake wakati mii si mwelewi.Sasa basi kwa sababu ss ni wanajamii naamini hakuna kitakachoharibika,Naomba anaefaham alphabeti (A-Z) kwa lugha ya alama anijuze ili nikirudi mjomba asione kama namchunia.Nimejaribu kupitia BAVITA mtandaoni labda ntakuta hata vidole vtatu vinamaanisha nini lkn sijfanikiwa kile nilichokitarajia,nikasema labda nimtafute ticha wa lugha ya alama hapa mtaani kwetu haijawa kazi rahisi.
 
Wana jf.
Juzi nimetembelewa na mtoto wa dada angu,sasa huyu mjomba ni bubu,sasa kwa siku mbili hizi nilizoo kaa nae,yaani hatari.
Kwanza anaonekana mwongeaji sana (kwa lugha za Alama)
Pili ni ananipenda sana muda woote yupo karibu na mimi labda kutokan na nilivyoondoka alikuwa mdogo sana.
Sasa kasheshe linakuja kwenye mawasiliano.
Mara akunje ngumi,mara aonyeshe vidole vitatu,mara viwili kama chama flani hapa TZ.Mara ashike kidevu japo hili nafahamu kuwa ni jinsia ya kiume.
Sasa amenifanya niwe nachelewa kurudi nyumbani,kwa kuhofia nikifika sitting room ataanza mwembwe zake wakati mii si mwelewi.Sasa basi kwa sababu ss ni wanajamii naamini hakuna kitakachoharibika,Naomba anaefaham alphabeti (A-Z) kwa lugha ya alama anijuze ili nikirudi mjomba asione kama namchunia.Nimejaribu kupitia BAVITA mtandaoni labda ntakuta hata vidole vtatu vinamaanisha nini lkn sijfanikiwa kile nilichokitarajia,nikasema labda nimtafute ticha wa lugha ya alama hapa mtaani kwetu haijawa kazi rahisi.

Jaribu kugoogle mkuu utapata somo kutoka sehemu kibao tu, nimejaribu kusearch "sign language" zimetirirka za kutosha!
 
Nenda facebook, jaribu kumtafta Bill Bosco yupo dsm, au mtafte Aneth Bill Bosco, mara ya mwisho alipangwa kazi sengerema. Yeye ni bubu, alisomea udsm sociology, na mme wake ni sign lingua interpreter
 
nenda gooogle kuna lugha ya alama, coz ipo chavita, ya hapa Tanzania search gooogle tu andika llugha ya alama, au check sign language bt zipo za American, English, Finland and American alphabet zinaenda na kiswahil tofaut ni ndogo tu!!!!!!!!!
 
Ahsanteni kwa msaada wenu nimefanikiwa!!
 
Back
Top Bottom