1gb
JF-Expert Member
- Jun 30, 2013
- 2,199
- 2,859
Wana jf.
Juzi nimetembelewa na mtoto wa dada angu,sasa huyu mjomba ni bubu,sasa kwa siku mbili hizi nilizoo kaa nae,yaani hatari. Kwanza anaonekana mwongeaji sana (kwa lugha za Alama).
Pili ni ananipenda sana muda woote yupo karibu na mimi labda kutokan na nilivyoondoka alikuwa mdogo sana. Sasa kasheshe linakuja kwenye mawasiliano. Mara akunje ngumi,mara aonyeshe vidole vitatu,mara viwili kama chama flani hapa TZ.Mara ashike kidevu japo hili nafahamu kuwa ni jinsia ya kiume.
Sasa amenifanya niwe nachelewa kurudi nyumbani,kwa kuhofia nikifika sitting room ataanza mwembwe zake wakati mii si mwelewi.Sasa basi kwa sababu ss ni wanajamii naamini hakuna kitakachoharibika,Naomba anaefaham alphabeti (A-Z) kwa lugha ya alama anijuze ili nikirudi mjomba asione kama namchunia.Nimejaribu kupitia BAVITA mtandaoni labda ntakuta hata vidole vtatu vinamaanisha nini lkn sijfanikiwa kile nilichokitarajia,nikasema labda nimtafute ticha wa lugha ya alama hapa mtaani kwetu haijawa kazi rahisi.