Msaada: Maelezo kuhusu HIV na 72 hours after infections.

Msaada: Maelezo kuhusu HIV na 72 hours after infections.

Analyse

JF-Expert Member
Joined
Jan 19, 2014
Posts
17,637
Reaction score
47,413
Habari zenu madokta na msio madokta.

Week kadhaa zilizopita niliamua kujitoa mhanga na kwenda hospitali kupima HIV.

Nilienda kwenye vituo vya Angaza,maana nikitaka walau nipate na ushauri na maelezo tofauti tofauti kuhusu HIV.

Japo nilikuwa nadhani nina elimu ya kutosha juu ya ili gonjwa,lakini nikajikuta vitu vingi vinakuwa vipya kwangu.

Sasa kilichofanya niandike uzi huu ni pale yule mshauri alipotuelezea kuhusu watu ambao wanaweza kuwa wameambukizwa (au kuhisi wameambukizwa HIV) kwa bahati mbaya mfano aliyebakwa,aliyepata ajari n.k. Kwavile vijidudu vya HIV huweza kuonekana katika vipimo 3 months after maambukizi,so waliobakwa n.k ndani ya maaa 72 ya maambukizi huwa wanapewa vidonge flan ambavyo watavitumia kwa siku kadhaa na vidonge hivyo huweza kuwaondolea ilo tatizo.

Kiukweli hii taarifa ilikuwa ngeni kwangu na ikapelekea niwe na maswali mengi kichwani.

1. Huu ugonjwa hauna dawa,sasa hii ni nini??

2. Ukimeza hizi dawa,hawa HIV wanakufa au wanadhoofika tu??

(a) Kama wanakufa kwanini madaktari wasitumie formula hii hii ya hivyo vidonge ili kutuletea dawa kamili?
(b) Kama wanadhoofika tu,hiyo dawa inamsaada gani maana badae watarudi.

Ombi: Binafsi sio daktari,ila kupitia nyie madaktari naomba walau image ya huyo virus wa huu ugonjwa kama ipo. Maana nikikumbuka wakati nasoma Bios O level,tulikuwa tunachora picha za parasites wengi tu wanaoeleta magonjwa ikiwemo bacteria na virusi.

Natanguliza shukrani zenu. Natumaini mtanifumbua macho.
 
Mpaka sasa hivi ARV zina uwezo wa kuua wadudu wanaotembea kwenye damu. Kwakua HIV virus hana RNA ili kujitengenezea copy anajiunga na cell inayoweza kumpokea mwilini ambayo ni CD4, cell hii ni askari tuliye nae mwilini ambae anauwezo wa kupigana na maambukizi mengi tunayokumbana nayo. CD4 ikishaungana na HIV virus inakuwa shida kutambua kuwa HIV ni adui kwani anakuwa ameshajitengenezea copy zenye HIV. CD4 zinatokea kwenye sehemu moja karibu nyuma ya sikio sehemu inaitwa thymus ambako ndiko inakozalishwa ikihitajika mwilini. Kuteketeza HIV walioko. Huko mpaka sasa hivi ARV imeshindwa kuingia na kutokomeza lakini wanasayansi bado wanalifanyia kazi hili ikiwezekana kuzipa nguvu cell za mwili ziwe na uwezo wa kupigana na virus wa HIV na hivyo zitaweza kupenya mpaka kwenye hiyo sehemu ya thymus.

Hivyo basi unapokunywa dawa unakuwa unadhibiti virus kutoweza kutoka mafichoni na kushambulia mwili. Unaporuka siku za kunywa dawa pia unawafanya wawe sugu na mwisho dawa zinakuwa hazina madhara tena kwao.
 
Nenda kwa zile post za decreption utaelewa vizuri. Wao ndo wanatuua. Ukienda kunywa ma ARV yao
 
Mpaka sasa hivi ARV zina uwezo wa kuua wadudu wanaotembea kwenye damu. Kwakua HIV virus hana RNA ili kujitengenezea copy anajiunga na cell inayoweza kumpokea mwilini ambayo ni CD4, cell hii ni askari tuliye nae mwilini ambae anauwezo wa kupigana na maambukizi mengi tunayokumbana nayo. CD4 ikishaungana na HIV virus inakuwa shida kutambua kuwa HIV ni adui kwani anakuwa ameshajitengenezea copy zenye HIV. CD4 zinatokea kwenye sehemu moja karibu nyuma ya sikio sehemu inaitwa thymus ambako ndiko inakozalishwa ikihitajika mwilini. Kuteketeza HIV walioko. Huko mpaka sasa hivi ARV imeshindwa kuingia na kutokomeza lakini wanasayansi bado wanalifanyia kazi hili ikiwezekana kuzipa nguvu cell za mwili ziwe na uwezo wa kupigana na virus wa HIV na hivyo zitaweza kupenya mpaka kwenye hiyo sehemu ya thymus.
Kwahiyo unamaanisha zile dawa ndani ya masaa 72 zinawawahi HIV kabla hawajafika huko kunakozalishwa CD4?

Na vipi kuhusu ombi langu la image ya huyo kirus anayetutesa?
 
Kwahiyo unamaanisha zile dawa ndani ya masaa 72 zinawawahi HIV kabla hawajafika huko kunakozalishwa CD4?

Na vipi kuhusu ombi langu la image ya huyo kirus anayetutesa?
Ndani ya masaa 72 unaweza kuwawahi kabla hawajajiunganisha na cells za mwili na kuwateketeza kabisa. Hii ni njia ambayo imeleta matumaini kwa wengi.
Wakisha jiunga na cells ndiyo umebatizwa nao mpaka kifo kiwatenganishe.
 
Analyse, Post Exposure Prophylaxis (PEP). Ni dawa anazotakiwa kupata mtu ambaye anahisi amepata maambuziki ya Ukimwi. Zinatakiwa kumezwa haraka ndani ya Masaa 72 mara tu pale mtu anahisi amekuwa exposed na HIV. Ni kweli 'zinasaidia' sana kuzuia maambukizi endapo muhusika atatumia dawa hizo kikamilifu kama inavyoelekezwa; kwamba ndani ya masaa hayo 72 mtu anaanza dose ambayo mostly ni kidonge 1x1; or 1x2, hata hivyo tiba hii siyo 100% kwamba itazuia maambukizi. Sadly, mtu anaweza kutumia PEP Kits kikamilifu and still akapata maambukizi.

Key word" "ZINASAIDIA"

Lizy.
 
Nashkuru kwa taarifa mkuu. Je haiwezekani kuzitumia hizo hizo PEP kuwatibu waathirika wengine?
 
Sasa hizo dawa kwanini zisitangazwe vizuri watu wazijue. Na watu wahamasishwe kutumia. Nadhani kufanya hivyo maambukizi yatapungua au kuisha kabisa.
.
.
Ila ngono zembe itashamiri!
 
Back
Top Bottom