Msaada maelezo ya kutambua Chanjo ya kuku ya TATU MOJA kama imepoteza ubora.

Titicomb

JF-Expert Member
Joined
Jan 27, 2012
Posts
12,823
Reaction score
21,210
Tafadhali naomba msaada wa maelezo ya kutambua endapo chanjo niliyo nunua bado ina ubora au imepoteza ubora kwa kuharibika au kuchakachuliwa.

Kwa mujibu wa maelezo ya wagunduzi chuo Cha SUA chanjo hiyo imewekwa rangi maalumu kama indicator ya kuonaesha ubora au usalama wa chanjo.
Wanasema ikiharibika au ikiongezwa kitu rangi itabadilika.
Sasa nauliza rangi sahihi ya chanjo Safi no ipi na ikiharibika inakuwa rangi gani?

Swali la pili, chanjo hii inaelezwa inatunzika katika jotoridi la ndani ya nyumba yaani normal room temperature (25 degrees Celsius).
Mara nyingi ukienda kununua unakuta wamehifadhi kwenye baridi kali au barafu. Je, hii freezing temperatures haiwezi kujaribu chanjo?

Inaonekana wauzaji wengi kwenye Agrovet wamekariri chanjo zote zitunzwe kwenye freezing temperatures.

Naomba msaada wenu wataalamu na wafugaji wenzangu sababu mara nyingi chanjo hii haofanyi vizuri. Nahisi sababu ya namna ilivyo hifadhiwa.
Labda iligandishwa au ilikaa muda mrefu kabla ya matumizi.
Kwasababu unanunua ikiwa imelowa karatasi (leaflet) iliyopo kwenye chupa inaharibika hauoni tarehe ya kuhairisha matumizi (expired date).

Swali la tatu, chanjo hii inafaa kwa kanga, bata mzinga, bata wa kawaida?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…