Msaada. Makadirio ya kodi kutoka TRA

Msaada. Makadirio ya kodi kutoka TRA

guzman_

JF-Expert Member
Joined
Jan 27, 2016
Posts
1,268
Reaction score
2,330
Wakuu za leo.

Katika kupambana na maisha nikaamua kuanzisha duka la rejareja almaarufu la mangi mitaa ya hapa Mwanza.

Nikaenda TRA kusajili TIN bana jamaa wakakadiria kodi nilipe 250,000 kwa mwaka. Sasa yaani nimeshindwa hata cha kuongea nawaambia mimi kwa hii miezi miwili kwa siku hardly naweza pata 10,000. Ikiwa siku nzuri atleast naweza pata 15,000.

Hapo hujatoa pango, umeme n.k, Kwa mwezi unaweza ishia na faida ya 50,000. sasa hii kodi ya 250,000 wameitoa wapi. Hafu wanasema mauzo yangu kwa mwaka ni mil 9.6 aseee nimejuta.

Sasa nimeamua kuachana na hii biashara bora nishinde nalala tu. Mtaji wenyewe laki 6.

Je. wakuu hii kodi 250,000 ni reasonable Kweli?
Hafu mbona kama wao wamekaa tu wanakukadiria ili ufeli ubaki na umasikini wako.

Nimeanza namna ya kuacha hii biashara, Kodi ikiisha tu naenda zangu kulima. Sasa ni namna gani naweza sitisha hili kadirio.
Asante
 
Kuna elimu ya kodi wanatuficha.

Mtaji kuanzia 0- milioni 4 uwezi kukadiliwa kodi kwa kuanza ila utalipa malipo madogo kupata leseni isiyo kuwa na makadilio mpaka ikivuka malengo wakija kukagua kukuta umevuka mtaji uliowekwa.
 
Daah namimi nipo kwny mchakato wa makadirio haya sijui wataniambia kiasi gani asee
 
Kitu wanachoshindwa kuelewa wengi makadirio ya kodi hayafanywi na tra unafanya mwenyewe unapoanza biashara ndio maana unapewa fomu ya kujaza ya assessment, wao wataangalia mtaji wako na gharama ya pango unalolipa kisha wataangalia kama vimeoana na makadirio uliyojaza.
Njia rahisi ni kutumia wahasibu ila gharama za wahasibu ni kubwa.
 
Sio kweli. Unless ni kampuni. Hapo unaulizwa tu umaeanza na sh ngapi na mauzo yako kwa siku. Then wanaropoka utalipa laki 8. Then wanajifanya kukushushia mpaka 450,000 utakataa wee utasikia 250,000 kwa kukusaidia.
 
Ni kweli ila kwa sababu wengi hawajui wanapewa.makadirio ya ovyo hata.mimi nilipopata mtaalamu ndio akanifungua macho.
Kitu muhimu ni kuweka kumbukumbu za mapato na matumizi kitu ambacho wengi hawafanyi.
 
Sasa duka la mangi unauza ugoro unataka kuweka kumbukumbu mzee. Si kujichosha tu
 
Hesabu ni muhimu.ndio.maans wahindi wana.maduka.makubwa mjini lakini kodi wanalipa kidogo
Mimi nimeamua kuachana nayo. Soon nitaandika barua ya kusitisha biashara. 250,000 kwa mwaka ni kama 21,000 kwa mwezi. Hujalipa frem, umeme n.k sasa mi nafanyia kazi TRA.
Hafu kumbukumbu si mpaka uwe ulishaendesha biashara atleast kwa muda flani.
 
Mwanzoni unajikadiria mwenyewe, tulikadiriwa mara ya kwanza 1800000 kwa mwaka lakini baada ya kufanya makadirio kupitia kwa mhasibu ilishuka hadi 300000 kwa mwaka na yeye ndio alituambia makadirio tunafanya wenyewe hata tulipoyapeleka hawakubisha.
 
Hii ni kampuni boss. sidhani kama ni duka la mangi?
 
Nenda tra waambie huo mzigo haubebeki. Wakigoma waandikie barua kuwa unafunga biashara peleka kwa meneja wa Tra Mkoa
Nimewaeleza maafisa pale wote ni kama hawaelewi sidhani hata kama walishafanya biashara.
 
Wakuu za leo.
Katika kupambana na maisha nikaamua kuanzisha duka la rejareja almaarufu la mangi mitaa ya hapa Mwanza.
Nikaenda TRA kusajili TIN bana jamaa wakakadiria kodi nilipe 250,000 kwa mwaka. Sasa yaani nimeshindwa hata cha kuongea nawaambia mimi kwa hii miezi miwili kwa siku hardly naweza pata 10,000. Ikiwa siku nzuri atleast naweza pata 15,000. Hapo hujatoa pango, umeme n.k, Kwa mwezi unaweza ishia na faida ya 50,000. sasa hii kodi ya 250,000 wameitoa wapi. Hafu wanasema mauzo yangu kwa mwaka ni mil 9.6 aseee nimejuta.
Sasa nimeamua kuachana na hii biashara bora nishinde nalala tu. Mtaji wenyewe laki 6.
Je. wakuu hii kodi 250,000 ni reasonable Kweli?
Hafu mbona kama wao wamekaa tu wanakukadiria ili ufeli ubaki na umasikini wako.
Nimeanza namna ya kuacha hii biashara, Kodi ikiisha tu naenda zangu kulima. Sasa ni namna gani naweza sitisha hili kadirio.
Asante

Ingiaa hapa mkuu cheki turn over ya mwaka kwa bei ya chini www.tra.go.tz hapo utaona kama umeibiwa au la
 
Back
Top Bottom