Msaada: Makisio ya kodi na ushuru bandarini

karma

Member
Joined
Apr 21, 2022
Posts
26
Reaction score
38
Wakuu wazima?

Katika process za kutoa kontena bandarini, naomba mwenye uelewa anifungue macho hapa. Ni kodi zipi na asilimia ngapi hulipwa kwa kontena la 40HQ, mzigo ni machines za kiwandani, rawmaterials na packages.

Itapendeza kama nikipata mchanganuo wa gharama zote.
Natanguliza shukrani..
 
1. Ushuru wa Forodha:
Unategemea aina ya bidhaa, mara nyingi hutakiwa kulipwa asilimia kati ya 0% hadi 25% ya thamani ya CIF (Cost, Insurance, and Freight).

Kiwango kinaweza kutofautiana kati ya mashine, malighafi, na vifungashio kulingana na viwango vya forodha vilivyowekwa na serikali.

2. Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT):
VAT ni 18% inayohesabiwa juu ya jumla ya thamani ya CIF pamoja na ushuru wa forodha.

3. Gharama za Bandarini:
Hizi zinajumuisha ada za upakuaji wa kontena, uhifadhi, na usindikaji wa huduma nyingine bandarini.
Zitatofautiana kulingana na muda wa kuhifadhi, aina ya huduma, na bei ya huduma za bandarini.

4. Gharama za Clearing Agent na kusafirisha mzigo kutoka bandarini.

Hizi mtanegotiate na wahusika.

Ila nashauri umtafute agent mzuri na mzoefu atakupa majibu mazuri zaidi.
 
Yaani huu uzi wa maana hakuna wasomaji tuliochangia na mleta mada nae kaingia mitini.
Ila ungekuwa uzi wa ki na hamisa, ungekuwa umeenda page kadhaa. Inasikitisha sana kwakweli.
 
Wakuu wazima?

Katika process za kutoa kontena bandarini, naomba mwenye uelewa anifungue macho hapa. Ni kodi zipi na asilimia ngapi hulipwa kwa kontena la 40HQ, mzigo ni machines za kiwandani, rawmaterials na packages.

Itapendeza kama nikipata mchanganuo wa gharama zote.
Natanguliza shukrani..
Tafuta clearance agent. Kila bidhaa au mashine ina aina zake za kodi. Sio uniform or flat rates.
Mfano kuna vitu vina VAT vingine havina etc
 
mzigo ni machines za kiwandani, rawmaterials na packages.
Kila mzigo huwa na HS Code yake.
  • Tambua HS code za mizigo yako, kulingana na Packing list
  • Kisha tembelea
    Code:
    https://trade.tanzania.go.tz/
    1739765375337.png
Mfano:
1739765449423.png

  • Fuatisha maelekezo na chagua "clearance" kwa chini utaona huu calculator
1739765551546.png

Hapo utapata makdirio, Ila kwa hesabu kamili, fika kwenye ofisi husika watakusaidia.
 
Back
Top Bottom