1. Ushuru wa Forodha:
Unategemea aina ya bidhaa, mara nyingi hutakiwa kulipwa asilimia kati ya 0% hadi 25% ya thamani ya CIF (Cost, Insurance, and Freight).
Kiwango kinaweza kutofautiana kati ya mashine, malighafi, na vifungashio kulingana na viwango vya forodha vilivyowekwa na serikali.
2. Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT):
VAT ni 18% inayohesabiwa juu ya jumla ya thamani ya CIF pamoja na ushuru wa forodha.
3. Gharama za Bandarini:
Hizi zinajumuisha ada za upakuaji wa kontena, uhifadhi, na usindikaji wa huduma nyingine bandarini.
Zitatofautiana kulingana na muda wa kuhifadhi, aina ya huduma, na bei ya huduma za bandarini.
4. Gharama za Clearing Agent na kusafirisha mzigo kutoka bandarini.
Hizi mtanegotiate na wahusika.
Ila nashauri umtafute agent mzuri na mzoefu atakupa majibu mazuri zaidi.