Msaada: Makosa ya kisarufi katika hii sentensi

Gaspa ni mwizi,ameiba fedha zangu.
Makosa ktk sentesi yako
Mtu hawezi kukuiba kitu ambacho ni mali yako,

hapana blessed, mpaka useme umeibiwa lazima kitu aidha kiwe cha kwako, ama kiwe katika umiliki/udhibiti wako..tatizo hapo ni mkato baada ya neno, au badala ya kuweka mkato unaweza kusema kuweka neno "ambaye"
 
Huwezi kusema "Ameniibia fedha zangu" kiambishi "ni" katika "ameNIibia kimeshaua ulazima wa kuongeza neno "zangu" hivyo sentensi hiyo ina makosa katka ujenzi wa tungo yenyewe. Ungepaswa kusema;
I.Ameiba fedha zangu AU
2.Ameniibia fedha.
Katika sentensi 1, neno AMEIBA halina kiambishi cha urejeshi ndiyo sababu lipo neno ZANGU.
Katika sentensi 2 hakuna neno zangu kwa sababu ipo mofimu ya urejeshi "i".
ADA YA MASOMO LIPA KWA M-PESA
 
uko sahihi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…