Nitakupa 1,23 ambazo unatakiwa kuzifanya:
1. Kwanza kabisa hakikisha unafanya takwimu za mali zote mwanzoni (inventory count kwa kizungu), hakikisha unaaandika hiyo takwimu, maharage KG 50, mchele...
2. Kila mauzo yanapofanyika hakikisha unaandika chini na kurudi kwenye ile takwimu yako na kupunguza. Mfano mchele KG 5 zimeuzwa unakuja kwenye takwimu unapuunguza. Kila unaponunua unakuja kuongeza kwenye takwimu
3. Mwisho wa mwezi rudia tena kuhesabu, hakikisha vilivyopo kwenye duka vipo kwenye takwimu, kama kuna tofauti fanya utafiti kwa nini imetokea tofauti.
Rudia zoezi hili kwa miezi 3 kila mwezi bila kukosa. Baada utakuwa tayari unazo kumbukumbu.
Kinachofuata ni kufanya uchambuzi wa kumbukumbu zako, kwanza kabisa tazama kila bidhaa na aangalia inavyoouzika kwa mwezi. Mfano mchele kitumbo ulipochukua takwimu Mara ya Kwanza ulikuwa KG 20, ulipochukua mara ya pili ulikuwa KG 18, mara ya tatu KG 15. Maana yake ni kwamba Kitumbo hauziki na unakujazia usiku, kisheria vitu unavyonunua vinatakiwa kuisha ndani ya siku 21, ukienda miezi mitatu na mokororo yasio uzika ni kwamba UMEZIKA fedha, unachotakiwa ni kuuza kwa hasara ili urudishe pesa yako na usije tena narudia tena kununua hicho kitu.
Kinachouwa maduka mengi ni UMBUMBUMBU wa wenye maduka, anadhani kujaza mafremu yale ndio bishara, biashara ni mzunguko wa fedha kizungu Cash Flow. Unachotakiwa ni kugeuza inventory upesi iwe cash aka tasilimu na kisha ukanunue tena. Kujaza makarabrasha ili uonekane duka limejaa kisha yaishie kuexpire ni sawa na kutupa pesa mtoni.
Kwa maswali nicheki inbox.