Msaada: Mambo gani nifanye ili kusimamia maduka ya rejareja?

Msaada: Mambo gani nifanye ili kusimamia maduka ya rejareja?

regnaldshirima

Senior Member
Joined
Aug 18, 2014
Posts
124
Reaction score
78
Habari wana jamii...

Sikuweza kusomea masuala ya biashara kutokana umaskin wa familia. Na ningependa kwa anaefahamu masuala ya kusimamia biashara nini kinatakiwa napenda niwezeze isimamia biashara katika ubora unaostahili
 
Hapo tafta mganga mzuri tu especially mganga wa kimasai ! Atakupa njia nzuri ya kusimamia biashara
 
Funga kamera mlangoni na mbili ndani kila duka. Afu fuatilia mienendo yote jioni maana zitakuwa zinarecod.
 
duka gani la reja reja?? chakula, vifaa vya ujenzi, urembo au dawa za asili?? then kwa ufupi usimamizi wa mali huanza pindi pale mzigo unapokuwa unaingia dukani mpaka unapoisha.
hivyo basi kitu muhimu kuliko vyote ni kuwa na kumbukumbu ya mauzo na manunuzi yako, katika sehemu mbili tofauti, mfano uwe na daftari la manunuzi na mauzo katika manunuzi unandika kila ktu hadi gharama ya usafiri na manunuzi unaandika vitu vyote vilivyouzwa
sasa usimamizi mzuri ni kujua mzigo ulioingia leo unaisha lini na ukiisha ntakuwa nimepata faida kiasi gani?? Kwa uelewa wangu ninavyofanya
 
Nitakupa 1,23 ambazo unatakiwa kuzifanya:
1. Kwanza kabisa hakikisha unafanya takwimu za mali zote mwanzoni (inventory count kwa kizungu), hakikisha unaaandika hiyo takwimu, maharage KG 50, mchele...
2. Kila mauzo yanapofanyika hakikisha unaandika chini na kurudi kwenye ile takwimu yako na kupunguza. Mfano mchele KG 5 zimeuzwa unakuja kwenye takwimu unapuunguza. Kila unaponunua unakuja kuongeza kwenye takwimu
3. Mwisho wa mwezi rudia tena kuhesabu, hakikisha vilivyopo kwenye duka vipo kwenye takwimu, kama kuna tofauti fanya utafiti kwa nini imetokea tofauti.

Rudia zoezi hili kwa miezi 3 kila mwezi bila kukosa. Baada utakuwa tayari unazo kumbukumbu.

Kinachofuata ni kufanya uchambuzi wa kumbukumbu zako, kwanza kabisa tazama kila bidhaa na aangalia inavyoouzika kwa mwezi. Mfano mchele kitumbo ulipochukua takwimu Mara ya Kwanza ulikuwa KG 20, ulipochukua mara ya pili ulikuwa KG 18, mara ya tatu KG 15. Maana yake ni kwamba Kitumbo hauziki na unakujazia usiku, kisheria vitu unavyonunua vinatakiwa kuisha ndani ya siku 21, ukienda miezi mitatu na mokororo yasio uzika ni kwamba UMEZIKA fedha, unachotakiwa ni kuuza kwa hasara ili urudishe pesa yako na usije tena narudia tena kununua hicho kitu.

Kinachouwa maduka mengi ni UMBUMBUMBU wa wenye maduka, anadhani kujaza mafremu yale ndio bishara, biashara ni mzunguko wa fedha kizungu Cash Flow. Unachotakiwa ni kugeuza inventory upesi iwe cash aka tasilimu na kisha ukanunue tena. Kujaza makarabrasha ili uonekane duka limejaa kisha yaishie kuexpire ni sawa na kutupa pesa mtoni.

Kwa maswali nicheki inbox.
 
Back
Top Bottom