Msaada: Matatizo ya masikio

Baba JJ

Senior Member
Joined
Feb 15, 2013
Posts
194
Reaction score
98
Heshima mbele wanaJF,

Nimekuwa na matatizo ya masikio yangu kwa muda wa miezi sita (6) sasa. Siku moja nilikuwa natembelea maeneo ya machimbo, maeneo hayo mara nyingi wanakuwa wanatumia milipuko kwa ajili ya kupasua miamba. ulitokea mlipuko wa nguvu sana mpaka karibu watu wote eneo lile walishtuka sana. kwangu mimi haikuwa kushtuka tu,bali pia nilianza kusikia masikio yakiwasha kwa ndani, baadae nikaanza kusikia MILUZI na NIKIONGEA NAJISIKIA MWENYEWE (MWANGWI), masikioni kwangu. Hali hii iliendelea mpaka siku moja nikaenda Hosp ya TMJ kupata matibabu, wale jamaa nao wana gharama sana, maana kumuona DR. tu ni Ths 20,000/=, wakanipa dawa ambayo nilitumia kwa siku 14 bila mafanikio. Baada ya kutumia hizo dawa sikuona mafanikio yoyote, mpaka sasa hivi hali ni ileile. kwa kweli napata shida sana hasa wakati wa kuongea na mtu ana kwa ana, lazima nimuangalkie usoni ili nijue anachoongea, ama kusikiliza simu lazima niw
eke loudspeaker, hAli hii inanipa wakati mgumu sana, maana inakuwa hadi kelo kwa unaokuwa nao karibu.

Tafadhali wanaJF, msaada wa namna ya kuondokana na hili janga.

Nawasilisha.

 
mi
mwenyewe nina tatzo hilo karibu miaka miwili sasa nimetumia dawa nyingi
bila mafanikio ila nina mpango wa kwenda ST.FRANSIC HOSPITAL IFAKARA
TUWASILIANE PLZ 0766728326 ukituma sms ni vizur zaid
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…