Heshima mbele wanaJF,
Nimekuwa na matatizo ya masikio yangu kwa muda wa miezi sita (6) sasa. Siku moja nilikuwa natembelea maeneo ya machimbo, maeneo hayo mara nyingi wanakuwa wanatumia milipuko kwa ajili ya kupasua miamba. ulitokea mlipuko wa nguvu sana mpaka karibu watu wote eneo lile walishtuka sana. kwangu mimi haikuwa kushtuka tu,bali pia nilianza kusikia masikio yakiwasha kwa ndani, baadae nikaanza kusikia MILUZI na NIKIONGEA NAJISIKIA MWENYEWE (MWANGWI), masikioni kwangu. Hali hii iliendelea mpaka siku moja nikaenda Hosp ya TMJ kupata matibabu, wale jamaa nao wana gharama sana, maana kumuona DR. tu ni Ths 20,000/=, wakanipa dawa ambayo nilitumia kwa siku 14 bila mafanikio. Baada ya kutumia hizo dawa sikuona mafanikio yoyote, mpaka sasa hivi hali ni ileile. kwa kweli napata shida sana hasa wakati wa kuongea na mtu ana kwa ana, lazima nimuangalkie usoni ili nijue anachoongea, ama kusikiliza simu lazima niweke loudspeaker, hAli hii inanipa wakati mgumu sana, maana inakuwa hadi kelo kwa unaokuwa nao karibu.
Tafadhali wanaJF, msaada wa namna ya kuondokana na hili janga.
Nawasilisha.