Msaada: Matunda ya Mparachichi kupukutika

bhakamu

JF-Expert Member
Joined
Sep 6, 2016
Posts
813
Reaction score
787
Msaada tafadhali, miparachichi yangu imepukutisha matunda yote yangali machanga sana, shida nini na niitatueje wataalam?
 
Maelezo yako hayajajitosheleza

Je ni mara ya kwanza maparachichi hayo yanazaa au ulishawahi kuvuna matunda hapo awali?
 
Maelezo yako hayajajitosheleza

Je ni mara ya kwanza maparachichi hayo yanazaa au ulishawahi kuvuna matunda hapo awali?
Ni mara ya kwanza kiongozi sijawahi kuvuna
 
Ni mara ya kwanza kiongozi sijawahi kuvuna
Mara nyingi parachichi kwa mara ya kwanza kuzaa huwa yanapukutisha matunda karibia yote..hiyo ni kawaida ila inategemea na aina ya mbegu ...unaweza kushangaa yakabaki matunda machache au yasibaki kabisa ...ila mara ya pili utaanza kufurahia matunda kwa wingi...

Nina uzoefu kidogo kwa sababu nilipokulia kuna parachichi kwa wingi sana.
 
Shukrani sana mkuu Kwa kunitoa wasiwasi nilikuwa nawaza kuikata kabisa
 
Ni mara ya kwanza kiongozi sijawahi kuvuna
Hio ni Abortion... Mbolea yenye calcium imeadimika humo.

Tafuta mbolea yenye calcium kwa wingi utumie, ukumbuke uwepo wa unyevu kwenye udongo ni muhimu ili mbolea iyeyuke na kufyonzwa kwa haraka kupitia mizizi.

Zingatia,. Usiweke mbolea karibu na shina, Kama miti ni mikubwa weka umbali wa mita 1.5 mpaka 3 kutoka shina lilipo. Ukiichimbia vishimo na kuifukia, kuzunguka mti.
 
Asante mkuu .Sasa iyo mbolea niiweke lini maana Kwa Sasa miti Haina hasta tundra Moja.

Sent from my M10_Max using JamiiForums mobile app
 
Nakujibu kutokana na uzoefu wangu. Miti hudondosha maua na matunda ukikutana na stress yoyote ile. Inaweza kua ukosefu wa mbolea(calcium), mvua kubwa, ukosefu wa maji, wanyama na wadudu pia.

Parachichi yako uliipa huduma gani mpaka ikafikia hatua ya kupukutisha matunda? Tuelezee kwanza huduma uliyo ipa hiyo parachichi hadi hatua ya kupukutisha hayo matunda tupate picha halisi ya kujua shida ni nini
 
Tutajie jina ya mbolea

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…