Msaada maumivu makali ya tumbo

mselambaya

Senior Member
Joined
Jan 10, 2017
Posts
106
Reaction score
77
Habari zenu wakuu mimi ni kijana mwenye umri wa miaka 24 nasumbuliwa na maumivu makali sana tumboni hasa wakati wa usiku mwaka wa saba huu maumivu haya huwa kwa kipindi fulani alafu yanapotea ila safari hii tokea yamekuja yamekaa kwa muda mrefu sana inaelekea mwezi wa tisa huu sipati usingizi yananitesa sana usiku nilienda nikapima nikakutwa nina taifod,uti na minyoo nikapewa dawa lakini maumivu yako palepale.hivyo basi nitafurai sana ushauri wa kuweza kunisaidia kupona maradhi haya.
 
Mkuu umewahi Fanya ultra sound kujua kuna shida Gani?

Au una historia yoyote ya kufanyiwa upasuaji before?
 
Mkuu umewahi Fanya ultra sound kujua kuna shida Gani?

Au una historia yoyote ya kufanyiwa upasuaji before?
Sijawai kufanya ultra sound wala sijawai kufanyiwa upasuaji
 
Fanya kipimo hiki ili ujue nini kinakusumbua,......................
oesophagogastroduodenoscopy (OGD)
 
Fanya kipimo hiki ili ujue nini kinakusumbua,......................
oesophagogastroduodenoscopy (OGD)
Shukrani mkuu ntafanya hivyo,je hicho kipimo kinapatikana hospitali yoyote au?
 
Sio zote, kinapatikana hospitali chache za rufaa na uhakika hospitali za kanda na National hospital.
 
Mkuu pole sana ila jarbu kuchunguza mshipa wa ngiri (Chango). Mimi nilikuwa na tatzo kama lako yaani nilikuwa nikiugua tumbo ni wiki 2 ndo linakata na likitulia ni mwezi au miezi miwili hali inarudia, Nilizungua sana hospital lakini wapi ila kaja kunitibu mtu ambae hata sikudhania kwa miti shamba na sasa nilishapona japo hali hutokea pale tu napokumbana na baridi kali. Hivyo bora ucheki hilo.
 
Shukrani mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…