Nilianza kupata dalili kama hizi mwaka 2019, hususani wakati wa joto kali, au jua kali. Nikinywa maji maumivu yanakata. Mwezi July 2023, nikaenda hosipital, Dr akanishauri nipime haja kubwa, kipimo cha "H-pylo"= Hericobacterpylory. Nikakutwa na hao bacteria, nikaandikiwa dawa. Saizi sina tena hayo maumivu.
Bacteria hao wanapatikana kwa kunywa maji yasiyochemshwa, kula matunda yasiyooshwa vizuri nk.
Zaidi ya asilimia 90 ya wagonjwa wa saratani ya utumbo, wanakutwa na hao bacteria. Bacteria hao wanasababisha vidonda vya tumbo.
Tofauti na hapo, fanya vipimo zaidi huenda una mawe kwenye figo.