Msaada: Mbinu Kufukuza Nyoka mashambani

Msaada: Mbinu Kufukuza Nyoka mashambani

Mutensa

JF-Expert Member
Joined
Feb 20, 2009
Posts
421
Reaction score
92
Wapendwa,

Katika jitihada za kupambana na umaskini, nilichukua kakichaka ambako nakasafisha kwa ajili ya shamba na shughuli za ufugaji. Changamoto niliyokutana nayo ni kuwa:

1. Kuna vichaka vingi vinavyozunguka eneo hili kiasi kwamba hata nikisafisha bado majirani zangu wanabaki na vichaka
2. Eneo hili ni zuri sana lakini lina nyoka wengi.

Naomba kujua mbinu za kisayansi - chemicals, mimea ya kupanda kufukuza nyoka, etc ninazoweza kutumia ili niepukane na adha ya nyoka hawa.

Nitashukuru kupata michango iliyo makini.
 
Nguchiro atawalinda vipi wasitoroke shambani? Given kwamba hawatakuwa wamekaa sehemu moja tu hapo shambani
 
Hicho kichaka kipo maeneo gani sababu kuna mtaalamu wa kukamata nyoka.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums.
 
Hatua ya muda mfupi ni kunyunyizia diesel (au mafuta ya taa) kuzunguka eneo lako.

Unaweza kutumia sprayer kama hii hapa chini kwenye picha kunyunyizia diesel hiyo kuzunguka eneo lako.

Harufu ya diesel inawakera sana nyoka na wataenda mbali.

Ila itabidi urudie ku-spray kama mvua itanyesha, maana maji ya mvua yakapunguza harufu ya diesel.

Hand-Sprayer-NS-15A-.jpg
 
kapandikize wadudu waoitwa sangara. ni aina ya siafu na wanaishi kwenye vishimo wanavojichimbia wenyewe ardhini. hawa wadudu ni dhahama kubwa sana kwa nyoka. popote walipo nyoka hakanyagi
 
Tumia Oil chafu unaweza kuipata bure au kwa bei ndogo sana, nyunyiza kuzunguka shamba lako ila kikubwa usafi wa shamba ni muhimu sana, shamba likiwa safi nyoka wote watahama na pia fuga kuku wa kienyeji na uwaache wajitafutie chakula nje.
 
This also helps for sure
Hatua ya muda mfupi ni kunyunyizia diesel (au mafuta ya taa) kuzunguka eneo lako.

Unaweza kutumia sprayer kama hii hapa chini kwenye picha kunyunyizia diesel hiyo kuzunguka eneo lako.

Harufu ya diesel inawakera sana nyoka na wataenda mbali.

Ila itabidi urudie ku-spray kama mvua itanyesha, maana maji ya mvua yakapunguza harufu ya diesel.

hand-sprayer-ns-15a-.jpg
 
Kapandikize wadudu waoitwa sangara. ni aina ya siafu na wanaishi kwenye vishimo wanavojichimbia wenyewe ardhini. hawa wadudu ni dhahama kubwa sana kwa nyoka. popote walipo nyoka hakanyagi
Looks interesting lakini hao sangara nawapata wapi kaka hapa dar/pwani?
 
tafuta mmea wa mchaichai ni mzuri sana kuzuia nyoka pia ni lishe kwani hutumika kwenye chai na una ladha ya kuvutia . unapanda pembeni mwa shamba
Mkuu hii ni kweli?
 
tuanjifunza wengi hapo, thanks kwa wanaochangia kwa uzuri
 
tafuta mmea wa mchaichai ni mzuri sana kuzuia nyoka pia ni lishe kwani hutumika kwenye chai na una ladha ya kuvutia . unapanda pembeni mwa shamba
Kuna sehemu nimeona pia wanasema kuwa ukiupanda kama sehemu ya bustani unasaidia kuzuia mbu wasikaribie hilo eneo.
 
Hatua ya muda mfupi ni kunyunyizia diesel (au mafuta ya taa) kuzunguka eneo lako.
Unaweza kutumia sprayer kama hii hapa chini kwenye picha kunyunyizia diesel hiyo kuzunguka eneo lako.
Harufu ya diesel inawakera sana nyoka na wataenda mbali.
Ila itabidi urudie ku-spray kama mvua itanyesha, maana maji ya mvua yakapunguza harufu ya diesel.

Hand-Sprayer-NS-15A-.jpg

Huu ni uharibifu wa mazingira wa hali ya juu mno. Never do that, petrol au Diesel utakayospray itabakia kwenye udongo au majani na mvua ikinyesha itasombwa na kwenda mtoni ambako huziba layer ya juu ya maji na kusababisha vifo kwa vimbe wa majini.

Nyoka sio adui yako kama yuko shambani, cha kufanya chunguza ni aina gani ya nyoka wanaoonekana mara kwa mara. Kama ni nyoka yoyote tofauti na Black Mamba, usijali, endelea na shuguli zako na hao nyoka watahama kwa kuona ongezeko la shuguli za binadamu. Kama Black Mamba angekuwa ameishaleta madhara. Ukishindwa kabisa ziko dawa za kufukuza nyoka ambazo ni environmental friendly ukienda kwenye maduka ya dawa utazipata. TAFADHALI USITUMIE DIESEL AU PETROL
 
Back
Top Bottom