Msaada mchanganyiko Wa lishe unaorejesha nguvu za kiume

Msaada mchanganyiko Wa lishe unaorejesha nguvu za kiume

Hili tatizo limekuzwa na wale maatibu wa tiba mbadala iliwapige pesa wa watu, chamsingi punguza stress unapofanya tendo la ndoa, uwe unaingatia lishe bora pia afya iwe maridadi yaani hauumwi presha wala kisukari au magonjwa yamoyo


Na mazoez ya mwili nayo muhim sana sana
 
Labda hoja yankupunguza stress ni bora zaidi nadhan ndo tatz mm 2013 nlkua na stress sana sikuweka kupiz bao 2 au 3 ila badae nlipataga hela hadi saiv napiga mpepe vzri

chamsing tutafute hela sana mana ndo znakoanzia stress
 
Wakuu alumelunda na msondomba

Mazoezi ya Kegel.
Nini maana ya Kegel ?

Kegel si kitu chochote zaidi ila ni kati majina mengine mengi maarufu kama Newton’s Law, au Murphy’s law na vivyo hivyo Arnold Kegel ambaye ndiye aliyevumbua mazoezi haya ya misuli ya sakafu wa kiuno (pelvic floor muscles) na kuyapa jina lake, ambapo Arnold Kegel ndiye hasa aliyevumbua faida za maoezi haya mnamo mwaka 1948.

Mazoezi ya Kegel yameonesha mafanikio makubwa sana hasa kwa wagonjwa wenye tatizo la kutokwa na haja ndogo pasipo uwezo wa kujizuia na pia wajawazito wenye shida hii pia. Kadharika ni tiba kwa wanaume wasioweza kukocontrol ufungaji wa magoli wakiwa uwanjani.

Zoezi hili ni rahisi sana na huenda huwa tunalifanya wakati wote na kila siku maishani labda tu ni kwasababu hatufahamu nini tukifanyacho na faida zake, basi tuone ni jinsi gani ya kufanya zoezi la Kegel, ambalo kimsingi husaidia kuimarisha misuli iliyopo chini ya kibofu cha mkojo.

Zoezi la Kegel kwa Wanaume na jinsi ya Kufanya.
Kegels ni zoezi ambalo ni rahisi sana kulifanya hasa pale utakapo bainisha hasa ni misuli gani husika, na njia mojawapo nyepesi ya kubainisha misuli hii ni wakati ule unapokwenda haja ndogo.

Njia au jinsi gani ya kutambua;
·Jaribu kuzuia mkojo wakati umeshaanza kukojoa au kama unatoka kwa kasi punguza kidogo kasi ya utokaji wa haja ndogo/mkojo.

·Zingatia kutokukaza misuli yako ya makalio, miguu, au tumbo na wala usizuie pumzi, wakati wa kufanya jaribio la kubainisha misuli hii husika.

·Endapo utaweza kupunguza kasi ya kutoka kwa Haja ndogo/mkojo au kuuzuia usitoke, hapo utakuwa umefaulu kubainisha haswa wapi ilipo misuli husika ifanyayo kazi hii na hii ndiyo huanyiwa zoezi la Kegel.

Baadhi ya watu wamebainisha misuli hii pale wanapovuta taswira ya kuzuia hewa kutoka kwenye njia ya haja kubwa na endapo utafanya hivi kwa misuli sahihi basi utapata hisia za kuvutika kuelekea ndani (pulling sensation) na hapo utaukwa umepata misuli hasa ya kiuno ipaswayo kufanyiwa zoezi hili, pia ni muhimu kuzingatia kufanya zoezi kwa misuli husika na wala si vinginevyo. (Some men need biofeedback to help them target the right muscles.)

Jinsi ya Kufanya Zoezi:
  • Kaza misuli hii taratibu na uhesabu taratibu moja mpaka tano.
  • Legeza tena Misuli hii taratibu kwa kuhesabu taratibu moja mpaka tano.
  • Rudia vivyo hivyo mara kumi 10.
  • Fanya Seti Kumi za Zoezi la Kegel mara Tatu kutwa kwa Siku, ikiwa na maana kuwa utafanya mara thelasini kwa siku.
Ukiwa ndiyo unaanza zoezi hili kwa mara ya kwanza yaweza kuwa rahisi kwako kufanya zoeizi umelala kupunguza ukinzani wa nguvu za uvutano( gravity) na inaweza kuwa rahisi pia kukaza misuli kwa Muda wa dakika mbili mpaka tatu tu awali.
Baada ya wiki chache baada ya kuanza zoezi ongeza muda wa kukaza(contract) misuli taratibu mpaka kufikia hesabu za taratibu kufikia tano au kumi na ufanye zoezi ukiwa umesimama, maana Kwa kusimama utaongeza uzito zaidi katika misuli yako ya sakafu ya kwenye kiuno na kufanya jitihada ya kuimarisha Uthibiti wako wa mkojo na Hali ya kuwahi kufika kileleni mapema. Kumbuka kutokukaza misuli yako ya makalio, miguu, wala ya tumbo wakati wa kufanya Zoezi la Kegel.

Ni wakati gani Utaanza uona Matokeo ya Zoezi la Kegel?
Ili kuona matokeo ya zoezi kwa kila zoezi ualolifanya kawaida huchukuwa Muda hivyo ni vyena kuwa na uvumilivu, ukiwa unafanya zoezi hili la Kegel Mara Tatu kutwa kwa siku utaweza kuona matokeo mazuri ndani ya wiki tatu mpaka sita, lakini kuna baadhi ya watu huona mapema zaidi. Jitahidi kuweka kumbukumbu kila ufanyapo tendo na hii itakuwa ya msaada sana kugundua mabadiliko na maendeleo ya zoezi.

Kama hujaweza kuona mabadiliko yoyote ndani ya mwezi mmoja, huenda labda bado hujafanikiwa kubaini hasa aina ya Misuli inayopaswa kufanyiwa zoezi husika la Kegel na hivyo ni vyema ukaanza juhudi upya za kuutafuta msuli husika.

Tips/Dondoo za jinsi ya kukusaidia kufanya Zoezi la Kegel sehemu ya Mazoea ya kila siku.
Moja ya Mazoezi yenye faida zaidi ni pale utakapofanya mara zote na wakati wote na ili kukusaidia kufanya hivyo jaribu kufuata dondoo hizi:
  • Jiwekee kanuni; fanya zoezi la Kegel wakati huohuo kila siku, mfano zoezi la kwanza ni asubuhi wakati unapiga mswaki na jioni wakati unaangalia taarifa ya Habari.
  • Kumbuka faida zake; kama utaendelea na zoezi la Kegel amini litaleta mabadiloko makubwa katika hali ya kuzuia mkojo usitoke wenyewe na kukufanya uweze kujizuia kufika kileleni mapema.
Ukilimudu vyema hili zoezi utakuwa na uwezo wa kuamua muda gani ufunge goli na upi usifunge. Hata hata ukifunga goli uume hausinyai na kupoteza ubora wake.

cc: MBITIYAZA
Lazima uwe umebanwa na mkojo mkuu?
 
Kwa msaada zaidi tena wa bure....just ni pm nikupe namba kuku instruct....rememb. Its free.
 
1. Fanya mazoezi.
2.Punguza mawazo unapokuwa kwenye mtanange, concetrate kwenye hilo suala tu. Pia jitahidi usiwe na hofu.
3. Kula vizuri hasa vyakula vya asili. Punguza junk food.
4. Fanya zoezi la kegel
5. Changanya maji ya limao, tangawizi na asali. Kunywa vijiko vitatu asbh na vi3 jioni. Haipiti siku 4 utaleta majibu.

Kila la kheri mkuu.
Asante mkuu...naanza kulifanyia kazi usiku huu.
 
Back
Top Bottom