Msaada mdogo wa NGOs mdogo wangu kazaliwa na maambukizi ya UKIMWI.

tamuuuuu

JF-Expert Member
Joined
Mar 10, 2014
Posts
21,329
Reaction score
28,063
Ni inaniuma Sana Sana nikimwangalia dogo.Nimehakiki kuwa ni kweli dogo amezaliwa na maambukizi.Sasa naomba msaada wa kama wa uangalizi wa karibu na huduma.Ndo Kwanza yupo darasa la pili. Yupo Mbeya.NIMEUMIA SANA.
WITO:
Jamani tuwe makini Sana hasa ktk kuwasababishia hawa malaika matatizo yasiyowahusu.
Asanteni sn.
 
Pole mkuu ila tambua kuwa na HIV sio death penalty,inasikitisha tunaishi dunia ya tatu ila jitahidi lishe yake iwe bora,more protein,vitamins less vyakula vya wanga na saturated oils,tembea kidogo mkuu fika hapo Botswana au Namibia or even SA katafute vitamins kwenye maduka ya dawa ya kueleweka,na pia pata ARVs ili awe anatumia,wenzetu hawa sasa ni kidonge kimoja kwa siku ,ila usisahau kuondoka na ripoti yake ya afya.Good luck
 
Asante sn Kwa ushauri wako mzuri mkuu nitazingatia.Ndo maana natafuta namna ili aweze kupata msaada madhubuti ktk hili.Me pia nitapambana dogo apate huduma lakini kama nikipata msaada wa NGOs ili apate huduma Bora.Ni mdogo eti jamani daaa Yana Baba!!!!!
 
serikali iimarishe huduma za afya na kutoa elimu, inakuwaje mtoto anazaliwa na maambukizi zama hizi??? anyway we mpeleke tu hospitak mfuate taratibu aanze dawa mapema ataishi vizuri tu mpk kuja kutimiza ndoto zake
 
serikali iimarishe huduma za afya na kutoa elimu, inakuwaje mtoto anazaliwa na maambukizi zama hizi??? anyway we mpeleke tu hospitak mfuate taratibu aanze dawa mapema ataishi vizuri tu mpk kuja kutimiza ndoto zake
Sawa mkuu,nimefuatilia ameanza dawa.Ila huduma za karibu na lishe ndo si nzuri kwakweli ndo maana ninatafuta msaada.
 
NGOs wanategemea fedha za wafadhiri pia ni miradi ambayo ina muda maalum..je umefikiria kama ukipata msaada wa NGO na ikatokea hiyo project ime-phase out itakuaje? Anyway.nakushauri nenda kwa Afisa Ustawi wa Jamii wa Wilaya / Manispaa kwa ushauri zaidi au nenda moja kwa moja hospitali ya mkoa utakutana na wataalamu wa hayo mambo na watakupa ABC za namna ya kufanya...kumbuka kuwa na UKIMWI haimaanishi ndio mwisho wa maisha kwani huyo dogo anaweza akafika mpaka chuo kikuu na bado akawa fit
 
Pole sana. inauma pale unapopata taarifa ya mtu kwenye familia anaumwa. Hongera kwa kuamua kuchukua utaratibu wa kuanza kumpatia mwongozo mapema
Baadhi ya NGOs nyingi siku hizi yenye miradi kuhusiana na HIV imemaliza muda wake
 
Pole sana. inauma pale unapopata taarifa ya mtu kwenye familia anaumwa. Hongera kwa kuamua kuchukua utaratibu wa kuanza kumpatia mwongozo mapema
Baadhi ya NGOs nyingi siku hizi yenye miradi kuhusiana na HIV imemaliza muda wake
Nawaza Sana Sana dada.Kiukweli anatumia dawa,Ila natafuta awe ktk mikono salama zaidi
 
Pole sana ndugu,umetoa ujumbe mzito sana kwa wanandoa mungu akubariki.Cha msingi nenda na huyo malaika kwa madaktari watakupa ushauri zaidi,Mungu awabariki.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…