Msaada: Mdogo wangu anahitimu Darasa la 8 Kenya. Je, anaweza kupata nafasi shule za serikali Tanzania?

Supu ya kokoto

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2013
Posts
4,194
Reaction score
7,602
Wakuu salama?

Nina mdogo wangu anasomea Kenya kwa ufadhili wa kanisa sasa mwaka huu anahitimu darasa la nane. Nilitaka akimaliza aje aendelee huku na masomo ya sekondari. Naomba kujua yafuatayo:

1. Inawezekana yeye kuhamia katika mfumo wa elimu ya Tanzania?
2. Ni taratibu zipi zifuatwe ili akidhi vigezo vya kujiunga na sekondari huku?
3. Je anaweza kupata nafasi shule za serikali?

Mawazo yenu wadau.
 
Inawezekana ila private. Mbona kuna niliosoma nao private waliishia std 6 wakaanza form 1?
 
Kuja kujiunga form 1 Tanzania government school ni ngumu, labda arudie darasa la 7 huku akifaulu ndo ataanza form 1 government school..

Km una pesa aanze form 1 kwa shule za binafsi hakuna pingamizi ni wewe tu na pesa zako.

Au nenda kwa mkuu wa sekondari akupe jina la mwanafunzi ambaye ameacha au hakuripoti shule iliko jina lake

Sent from my SM-M115F using JamiiForums mobile app
 
Mkuu asante ila hiyo option ya kwenda kwa mkuu wa shule haiwezi kuwa na athari mbeleni
 
Mara paap hiyo option ikagonga mwamba....
Inaweza kugonga mwamba maana siku hizi mambo yako advanced tofauti na zamani. La saba data zao zipo online na mamlaka kuanzia picha mpaka matokeo. Ni bora akajiridhisha kwanza kama ulivyoshauri
 
Asante mkuu,
 
Inawezekana.. lakini itakubidi kufuata utaratibu..
Sio kweli kwamba unaweza kumuingiza mtoto shuleni (private/government) bila kufuata utaratibu..
Kwasasa Kuna namba mtoto anapewa toka shule ya msingi Hadi sekondari..
Kama unataka kumuingiza shule za Tanzania itakubidi kuleta matokeo ya mitihani ya huko kenya..kwa maelezo zaidi..nenda ofisi ya afisa elimu atakusaidia
 
Hapana kuna option ya kubadilisha jina kabla ya registration kwaajili ya mtihani wa national form 2
Jina halibadilishwi hata likikosewa. Siku hizi hakuna usajili wa karatasi na faili. Kila kitu ni mtandaoni. Na jina halibadiliki zaidi ya herufi moja au mbili tu. Mfano Jacklina ndo inaweza kuwa Jacklin basi.

Utaki acha.
 
Back
Top Bottom