Msaada: Mdogo wangu anahitimu Darasa la 8 Kenya. Je, anaweza kupata nafasi shule za serikali Tanzania?

Msaada: Mdogo wangu anahitimu Darasa la 8 Kenya. Je, anaweza kupata nafasi shule za serikali Tanzania?

Wakuu salama?

Nina mdogo wangu anasomea Kenya kwa ufadhili wa kanisa sasa mwaka huu anahitimu darasa la nane. Nilitaka akimaliza aje aendelee huku na masomo ya sekondari. Naomba kujua yafuatayo:

1. Inawezekana yeye kuhamia katika mfumo wa elimu ya Tanzania?
2. Ni taratibu zipi zifuatwe ili akidhi vigezo vya kujiunga na sekondari huku?
3. Je anaweza kupata nafasi shule za serikali?

Mawazo yenu wadau.
Peleka private.
Mtoto hayupo ktk data base.
Au nenda wizarani.
 
Aenedelee tu hukohuko
Amebakisha miaka 4 tu aanze University
Akija huku ni 6 mingine, na ukiongeza miaka 8 aliyosoma, anapoteza miaka 3 katika maisha yake
 
Back
Top Bottom