Langu
Member
- Nov 20, 2011
- 37
- 9
- Thread starter
-
- #21
Vipi Kama hamjafunga ndo a ila mmeishi miaka mingi
Na kuchuma Mali pamoja na sasa mnataka kuachana?
Kama mmeishi kuanzia miaka miwili na kuendelea japo hamna ndoa, na watu wakaichukulia hiyo kama ndoa kwa waliokuwa wakiwaona, hii italeta dhanio la kisheria kuwa hiyo ni ndoa, naomba nieleweke si ndoa, ni dhanio tu kuwa ni ndoa lengo kubwa ni pamoja na,
Kama kuna watoto mmezaa pamoja, wapate haki zao kutokana na hayo mahusiano yaliyokuwepo, pili kama kuna mali mlivuna wote muweze kugawana.
Ila, mpaka mahakama ifikie maaumuzi ya kuweka dhanio la ndoa, mpaka kuwepo na ugomvi kati yenu na mda niliotaja hapo juu umefika.
Huwezi kwenda kuiomba mahakama ugawiwe chako kwa kigezo kuwa unataka ugawiwe tu alikuwa mume wako, na mlichuma wote wala hamna mgogoro.
Mwingine anaweza kuongeza au kurekebisha, angalia Sheria ya Ndoa ya 1971 kifungu cha 61.