Msaada, Mgao Wa Mali Endapo Wanandoa Wametalakiana?

Msaada, Mgao Wa Mali Endapo Wanandoa Wametalakiana?

Vipi Kama hamjafunga ndo a ila mmeishi miaka mingi
Na kuchuma Mali pamoja na sasa mnataka kuachana?

Kama mmeishi kuanzia miaka miwili na kuendelea japo hamna ndoa, na watu wakaichukulia hiyo kama ndoa kwa waliokuwa wakiwaona, hii italeta dhanio la kisheria kuwa hiyo ni ndoa, naomba nieleweke si ndoa, ni dhanio tu kuwa ni ndoa lengo kubwa ni pamoja na,

Kama kuna watoto mmezaa pamoja, wapate haki zao kutokana na hayo mahusiano yaliyokuwepo, pili kama kuna mali mlivuna wote muweze kugawana.

Ila, mpaka mahakama ifikie maaumuzi ya kuweka dhanio la ndoa, mpaka kuwepo na ugomvi kati yenu na mda niliotaja hapo juu umefika.

Huwezi kwenda kuiomba mahakama ugawiwe chako kwa kigezo kuwa unataka ugawiwe tu alikuwa mume wako, na mlichuma wote wala hamna mgogoro.

Mwingine anaweza kuongeza au kurekebisha, angalia Sheria ya Ndoa ya 1971 kifungu cha 61.
 
wazazi wangu mahakama imewapa talaka,hawa walikuwa wafanyakazi,kila mmoja na kituo chake.ni wanandoa wenye cheti.mzee alimtelekeza mama kwa miaka 11,mama hakuolewa ila mzee akawa na mke ambae si wakisheria maana ni wakristo..sasa ishu ya mgao itakuwa vipi hapo maana mzee alikokuwa huko kuna mali,japo alizinunua peke yake,na kwa bi mkubwa nako zipo nazo aliganga kivyake.lakini mahakama ilikuwa haijatoa talaka. Je mali hizi zinahesabika walichuma pamoja kisheria

nb.muda wote huu mama aliishi na watoto na dingi alikuwa cngle tu!
 
BI. HAWA MOHAMED v. ALLY SEIF [1983] TLR 32

Ni hukumu muhimu na maarufu kuliko zote pale linapokuja suala la migogoro ya wana-ndoa wanaotaka kutalikiana na pia suala zima la ugawanaji mali pale mahakama inaporidha talaka itolewe na ndoa hiyo ihesabike kwamba imeshindwa kuhimi mikikimikiki ya kutoelewana. nazungumzia hapo tamu inayogeuka kuwa shubiri baadaye.

Hukumu huu ilitolewa mwaka 1983 na Jopo la Majaji Watatu wa Mahakama ya Rufaa Tanzania (Jaji Mkuu Nyalali, kama alivyokuwa wakati ule, Jaji Lewis Makame na Jaji Robert Kisanga). Mengi yalizungumzwa humo na kinachoskikitisha hata baadhi ya wanasheria wameilewa vibaya hukumu hii kwa kutoisoma kwa umakini neno kwa neno, aya kwa aya.

Inatosha tu kusema kuwa kikubwa kilichoelekezwa hapo ni kwamba mama wa nyumbani anastahili kupata mgawo katika mali iliyochumwa na wanandoa hata kama kazi alizofanya ni za nyumbani tu na mumewe haijalishi alikuwa akikesha akirusha ndege, katika vikao vya mawaziri, kwenye dili kubwa ama safari za ki-biashara ana kazi nyinginezo, iweza kitaalam ama za suluba. Nikumbushe tena, jambo hili lisieleweke kijumla jumla tu hivyo, mahakama ilitoa ufafanuzi zaidi katika hili na sitaweza kutazungumza yote hapa.

Kesi hii ni muhimu kwa vile Mahakama hii ikiwa ni ya Juu zaidi Kikatiba na ambayo hukumu zake zapaswa kufuatwa na mahakame zote chini yake (katika tafsiri ya sheria husika). Ndiyo kusema,Jaji wa Mahakama Kuu, Hakimu wa Mahakama ya Wilaya au Ilala na wengineo wanatarajiwa kuzingatia msingi uliwekwa hapo.

Noma sana, maelezo haya nilikopi mahali halafu nikayatoa kama yakwangu, aibu kweli kweli.

ELIMU YA SHERIA (DENIS MARINGO): HUKUMU YA HAWA MOHAMED v. ALLY SEFU [1983] TLR 32 INAHUSIKA NA NINI?
 
Mkuu,mkishakaa miaka 2 ndani ya paa moja,kisheria ninyi ni mke na mume.japokuwa mkikaa miezi 6 watu wanaizungumzia kuwa mshakuwa wanandoa ni sawa,ila mkiachana hamuwezi kwenda sheriani,maana huko wanasikiliza waliokaa pamoja kuanzia miaka 2 na kuendelea.

Ingawa section 160 sub 2 LMA inarebat hii presamption mkuu na nicourt pekee inayoweza pressume kama kulikuwa naprissamtion ama hapana hata kama vigezo vyote vpo.though kuna shool of thought mbil znakinzana ambyo moja inazungumzia stil ndoa inaweza kuwa valid bila kujali hyo section nliyoitaja hapo juu kwakuzingatia section 41 ya LMA
 
Back
Top Bottom