Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mkuu wapi nitapata hawa madaktari wa mifupa?Pole sana kwa hayo matatizo yako ushauri mzuri nenda kwanza Hospitali kawaone Ma-Daktari wahusika wa mifupa wakupime na kukutibu. Ikishindikana njoo hapa utpe Feedback tutakupa ushauri mzuri mwengine asante pole sana mkuu.@is3haq
Mkuu wapi nitapata hawa madaktari wa mifupa?
Habarini wana jamvi, mimi ni kijana wa miaka 23 nina tatizo katika mguu wangu wa kushoto.Kuanzia kwenye goti kushuka chini kuna muda unapoteza hisia, wiki ya pili sasa tatzo hili linanisumbua.
Naombeni ushauri wenu.
Nenda Hospitali Kuu ya Muhimbili utapata hawa Ma-Daktari wa mifupa g.n.nMkuu wapi nitapata hawa madaktari wa mifupa?
vipi mkubwa ulienda hospitali? Mi mwnyw nina tatizo hilo. Umeshapata suluhisho?
Nashukuru kwa mawazo yenu wanajamvi, nilienda hospital pale Herbat Kairuki na dokta akanieleza nini kinanisumbua, tatizo lilikuwa kuna nerve za fahamu zinazoleta taarifa kwenye mguu zilibanwa maeneo ya nyonga kutokana na kukaa chini muda mrefu.
Nilipewa vidonge vya kumeza na alishauri nifanye mazoezi especially ya kuruka kichurachura na yamenisaidia sana. Hivi sasa tatizo kama linaelekea kuisha.
Ushauri kwa wote tunaofanya shughuli za kukaa sana chini tutenge muda wa mazoezi japo wa dakika 30 ili tuepukane na matitzo yasiyo ya lazima.