Msaada: Mifuko ya dhamana UTT (Umoja Fund n.k)

Msaada: Mifuko ya dhamana UTT (Umoja Fund n.k)

regnaldshirima

Senior Member
Joined
Aug 18, 2014
Posts
124
Reaction score
78
Ningependa kujua jinsi mifuko hii ya dhamana toka kwa Utt inavyofanya kazi mfano. Kununua vipande.kuuza vipande.kutoa fedha zako
 
Nimefungua account ya hii kitu UTT ila sijanunua unit bado.
Kufungua account ni unajaza form tu napewa account number yako, unaweza kununua units kupia CRDB au MPESA,Tigo-Pesa.

So kwa mfano leo unit moja ya Umoja Fund ni sh 458.6392 kununua so ukiweka 1 million unapata unit 1,000,000/458.6392 = 2180. Kuziuza always ni bei ya Unit - 1% ya bei so 454.0528 kwa leo.

Wana guarantee kuwa ukitaka kuuza units utapata hela zako ndani ya siku kumi.

Kutegemea na aina ya fund kunaweza kukawa na penalty kama ukiuza units baada ya muda mfupi, kwa mfano Watoto fund, kwa sababu hii lengo lake ni kumplipia mtoto shule huko mbeleni.

Bei ya unit moja inabadilika daily kutokana na vitu vilivyowekezwa kwenye fund hiyo so kwa mfano Umoja Fund ina hisa za TBL, CRDB, Bond za Serikali, Fixed deposits etc.

Kushuka au kupanda kwa investment yako kutategemea na hizo Hisa na Bond zinaperform vipi.


 
Back
Top Bottom