- Thread starter
-
- #21
Mimi sina shida na mali ya wazee wangu lakini najua kuwa mali za wazee inabidi wapewe wenye uwezo wa kuziendeleza(siyo uwezo wa kielimu bali fedha). Kuna watu hawatakiwi kupewa ijapokuwa wana haki ninajitafutia maisha lakini hata nikifa mali zangu nitawarithisha watoto wangu kadri ya uwezo wao. Siwezi kumpa mtoto ambaye hajawahi hata kujenga choo ghorofa, mtoto hajui hata tabu ya kugombana na mafundi na gharama za ujenzi. Utakuja kuamka huko kuzimu ndani ya miezi michache vitu vinauzwa vyote. Kama mzazi hajaacha wosia nashauri busara itumike waachiwe wenye uwezo wa kifedha waziendeleze ukipata gawio lako wekeza. Usijifanye kimbele mbele ili uonekane utangukia pua vibayya sana.
Hapa tunaongelea MIRATHI mkuu
Kwamba mwenye mali kafariki na kisheria wanarithi watoto
Nakuuliza kama Baba alikua na makampuni na mdogo wako alifanikiwa kuanzisha kampuni zake zikafanikiwa lakini wewe ukawa mwalimu mpintimbi primary school
Utapoteza haki zako kwasababu mdogo wako anahela na makampuni wakati wewe unahangaika na mikopo ya kausha damu kila mwezi
Usichanganye HAKI na uwezo wa kuendesha
Hakuna sheria inayosema mtu asipewe haki yake kisa ni masikini