Msaada; Misimu mbalimbali ya kilimo!!

Msaada; Misimu mbalimbali ya kilimo!!

Shakir

JF-Expert Member
Joined
Jul 31, 2012
Posts
1,627
Reaction score
1,926
Wadau,

Nimekua nikipitia jukwaa hili mara kwa mara, na ukweli hili jukwaa limenishawishi sana kua mkulima. Nimeshanunua Ardhi sehemu mbalimbali, iliyobaki ni kuanza tu kilimo.

Sasa basi, naombeni mnisaidie ni msimu gani ndio mzuri wa zao fulani. Mfano mahindi yanapandwa mwezi gani, maharagwe, Ufuta, mbogamboga kama Nyanya na Hoho, Matikiti, e.t.c.

Mimi kwa elimu yangu ndogo ya kilimo najuaga kila zao linapandwa January na kuvunwa June, lakini nimehisi pia inaweza ikawa sio!!

Mathalan, kama ni kweli mazao mengi yanavunwa June, nakwakua ardhi hizi nimezipata karibia na June, ina maana mshamba yatakaa idle mpaka January?

Ni mazao gani yanaweza kupandwa kuanzia mwezi huu hadi December? Sabasaba niliambiwa kuna Mahindi yanapandwaga October, lakini vipi kilimo kama cha matikiti,nyanya na vitunguu labda??

Mashamba yapo Kilwa 30acres, Kibamba 1Acre, Mlandizi 40 Acre na Kisarawe 30Acre. Ila hili la Kisarawe ni msitu kwa sasa so halifai for immediate use!!
 
pitia post mbalimbali zinazohusu kilimo.ila kw maeneo yako yote hayo lima ufuta sbb ufuta kwa ukanda huo wote unakubali.
 
pitia post mbalimbali zinazohusu kilimo.ila kw maeneo yako yote hayo lima ufuta sbb ufuta kwa ukanda huo wote unakubali.
Ahsante Kaka,

Ila kuna kitu Naomba unisaidie. Zao kukubali ni one issue, na kulipanda kwa wakati ni another issue. Tuseme huu wakati tuliopo hasa ni wakati/msimu wa zao gani kwa maeneo tajwa?

Ufuta unakubali ukanda huu wa pwani, lakini nikiupanda sasa hivi utaota?

Na kama msimu wake bado, nini nipande sasa wakati nasubiria hicho kipindi cha ufuta kikifika?

Na je nikiunganisha unganisha kilimo cha mzunguko kama hivi sintoichosha ardhi?

Msaada please!!
 
kwanza ningependa unamashamba ya umwagiliaji ktk mashamba yako hapo?km unayo unaweza ukalima sahvi ila c ufuta.unaweza ukalima nyanya kitunguu kwaujumla mazao ya bustani kw sasa.
 
hayo mashamba yako yaandae vizuri msimu wa ufuta ndyo huu unakuja,kusanya nguvu ulime hzo eka zote 120 ufuta,lima kwakufuata kanuni zote mbegu bora panda kwa mstari palilizi nadawa.kwahzo eka utapata faida kubwa sna.achana na shughuli nyngne zakulima kwa sahvi elekeza nguvu zako hapo na mandalizi yakulima yapo karibu c mbali.
 
Back
Top Bottom