Msaada: Mke wa mtu anataka kuhamia kwangu

Mwanamke mpumbavu hubomoa nyumba yake Mwenyewe.
Maisha yashaharibika hapo, familia imeshavunjika. There is times maisha yanapoteza maana , hasa yakikukuta.
 
Yaani una vitu vya kuhamisha na kirikuu ndio unachukuwa mke wa mtu. Pia uliposema tu unatumua card ya Mme mwenzio nikajua hunakitu Kwa hii tu unaweza pewa kesi picha zako ziko kwenye ATM ulizotoa pesa.

Kwa Sasa hama mji kabisa, badili na number otherwise ni swala la muda tu, na huyo manzi mshauli akae Kwa kutukia kwao jamaa ushahidi anao live.
 
Wanaume wasiokua na akili(vichaa) wanaongezeka kila siku na serikali ipo kimya.

NB:kula mke wa mtu hadi kwenda kulala kwake ni moja ya dalili ya udumavu wa akili.

Pia wanawake mjifunze ukiwa kwenye ndoa akaja mwanaume kua anakupenda sio kweli ni tamaa tu na usitegemee ukaachika akakuoa maana na yeye ataogopa kilichompata mwenzake.
 
Msaidie apate talaka, kabla ya talaka, mpe sapoti apate chumba chake, just make sure you support her. Baada ya talaka, subiri muda kati ya miaka miwili chukua mke. Kipindi hujamchukua hakikisha unakuwa nae karibu. Owa huyo mwanamke maana umemharibia wewe.
 
Hivyo nilikuwa naenda usiku kulala kwake na siku nisipoenda basi nilikuwa nampigia simu huyo mpenzi wangu tunazungumza hadi usiku wa manane.

pia nilimpenda mno mtoto wake mdogo, nilikuwa nampelekea vizawadi zawadi nikienda kulala, nacheza nako in short ni kacheshi mno kale katoto na kalinipenda pia.
 
Mali uliyokula kwa siri umeachiwa ujipakulie utakavyo, ushauri wa nini sasa!?
Mchuma janga....
 
Utajua kilichomnyoa Kanga manyoya, wewe badala ungekuwa unadokoa kwa siri sana mara moja moja uliamua kujimilikisha kabisa mke wa mtu!
 
1st of all umeharibu maisha ya huyo mwanamke, kubali ukatae hilo ni kweli.

2nd hapo naona only two options na katika kila option huyo mwanamke lazima ajute alichokifanya.

1st option ukubali kukaa nae huku akiendelea kupambania watoto wake ambao sidhani kama atapata full custody kulingana na ushahidi jamaa aliokuwa nao, pia mkikaa pamoja ataanza kukujua vizur na kadri siku zitakavozidi kwenda mtaanza kugombana, ataanza kujua wewe ni mwanaume wa design gani ambae hujisomi na hueshimu ndoa za watu.
Kwasababu kipindi cha nyuma mlikuwa mnakutana mkitaka kunyanduana ila mkikaa pamoja kwa muda mrefu ndo mtaanza kuchokana vizur, sasa hapo ndo utakapo jua wanawake ni watu wa aina gani.

Na hata ukikaa nae huyo mwanamke atakusaliti tuu na wewe, kwasababu kama kamsaliti mme wake wa ndoa kwann asikusaliti wewe??

2nd option ni wewe umkatae (uvunje mahusiano nae) kwasababu ya woga wako na kutokujiamini kwako, pamoja na mambo mengine uliyosema, ikiwa utachukua 2nd option huyo mwanamke atajuta, atakosa mme na atakosa na mpenzi (mtaka mawili vyote humponyoka) kiufupi katika option zote huyo mwanamke lazima ajute kumsaliti mme wake na kutoa uchi kwa mariooo.

N.B
Wanawake jifunzeni kitu kimoja, mme wako ndo anayekupenda na anayekuheshimu, mwanaume kakutoa kwenu kakuoa kakuleta kwake anakuhudumia kila kitu, unataka upendo gani zaidi ya huu??
Mwanaume kakutolea mahari ili akuoe uwe wake milele, hajataka ale mali ya watu bure, hapana, ameheshimu sheria, taratibu na kanuni, unataka heshima gani zaidi ya hii??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…