Msaada: Mke wa mtu anataka kuhamia kwangu

Astakafillah 😁😁😁😁😁
We jamaa una misimimo ya ajabu..
Huyo si kwanaume mwenzako khaaa
 
Daaaah wazee wa #KATAA #NDOA wanazidi kuongeza wafuasi
 
Jamaa nimemkubari, umechukua mkewe amekuachia kiroho safi
 
Kama unawinda wachawi unashindwa vp kumwinda huyo jamaa?...amin amin nakuambia huyo mwamba hatakuacha,he is going to hunt you Hata uende kuzimu na vile atakufanya bora ungewatukana wale wajeda wa lugalo!
 
Ungehangaika na bitcoin wala usingepata shida yote hii......
 
Ndugu zangu kabla sijaendelea kuna mambo machache nilitamani kuyasema:

Kwanza, unapomuona mtu amekuja kuomba ushauri JF unapaswa umshauri na sio kumtukana, kumkejeli na kashfa nyingine nyingi. Kila mtu anakosea, usijione wewe ni mkamilifu sana kiasi cha kuwa na haki ya kutukana wenzio.

Pili, kuna wazee wa kudai muendelezo hawa watu wanakera sana, unaomba ushauri, wao wanaomba muendelezo inamaana hata ukifa ni sawa tu kikubwa wao wapate muendelezo.

Tatu, napenda kuwashukuru wanajf wafuatao kwa ushauri wao Nuzulati DR HAYA LAND Wakilimkuu , laskaboza Lubebenamawe Excel na wengine wote walionipa ushauri ambao kwa namna moja au nyingine umeniwezesha mimi kuwa hapa nilipo leo.

Nyie wenye akili, msiokosea, Malaika watakatifu njooni tena mnitukane. Haiwezekani mtu anakutukana kama vile anakulisha… tuache mambo ya ajabu… kila mtu anakosea… kukosea kwangu kidogo kusifanye nionekane kama mimi ndo mkuu wa wenyedhambi….

…….. ……….. ……….

Tuendelee…

jana nilikamilisha mchakato wa kuuza vitu vyangu vyote, (usiombe uuze kitu ukiwa na shida mtu ananunua kama vile hataki, tena kwa bei anayotaka yeye…) niliuza mpaka simu yangu ya mkononi nikanunua nyingine, laini pia nimesajiri nyingine. Mara ya mwisho nimewasiliana na huyo mwanamke jana asubuhi, nikaahidi Kwenda kumuona, japo sikuthubutu Kwenda. Sasa niko kwenye gari, nimeamua kurudi kwanza nyumbani ili nijipange nianze mapambano ya kutafuta Maisha upya… sina mawasiliano na huyo mwanamke kwa sasa, japo namba zake ziko kichwani na sijui zitatokaje. Ila nimepanga niwe napeleleza taratiru na nikigundua kuwa mme wake amemuacha ki ukweli ukweli ntaenda tu nimtafute ili tuweze kuendeleza Maisha yetu Pamoja. Kusema kweli kuna chemistry Fulani nzuri sana kati yetu na naamini tutafika mbali… (japo namuomba Mungu amsaidie wayamalize haya mambo na mmewe and finally waishi vyema)

Samahani kwa wote ambao story yangu itakuwa imewakera kwa namna moja au nyingine ila ndo Maisha haya… pia NAOMBA MSAMAHA kwa mme wa mwanamke huyo iwapo atauona ujumbe wangu naomba anisamehe sana I know it hurt… (sometimes life lose its purpose and everything become a mess)

kwa mama jay (kipenzi changu) I chose to be your friend but falling in love with you was out of my control…


Rag’n’Bone Man -
Human
 
Akhasante sana mkuu kwa ushauri wako.
 
Kama unawinda wachawi unashindwa vp kumwinda huyo jamaa?...amin amin nakuambia huyo mwamba hatakuacha,he is going to hunt you Hata uende kuzimu na vile atakufanya bora ungewatukana wale wajeda wa lugalo
Naamini atanisamehe tu kaka....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…