Msaada: Mke wa mtu anataka kuhamia kwangu

Msaada: Mke wa mtu anataka kuhamia kwangu

Hakuna ujinga kama kujisifu kuchukua mke wa mtu, bado huwajui wanawake hata robo, iko siku utajuta, hawa ni viumbe wasiotafsirika wala kutabirika.
Sijajisifu na siwezi jisifu... Najuta tu mpaka sasa
 
yeye anadhani imeisha,hajui jamaa ana uchungu kiasi gani!wanaume wenzangu tuheshimiane maana kula mke wa mtu ni dharau kubwa na isiyovumilika kwa mwanaume!
Mungu atusamehe sisi inshallah
 
Hu
Mi sioni tatizo hapo mbona, maana umesema huyo mwanamke unampenda na mtoto wake ni mcheshi, mwanamke aende mahakamani adai talaka akubali alikuwa anachepuka atapewa talaka fasta then mtaendeleza kupigana miti, sometime mke wa kuishi nae unakuta kaolewa sehemu nyingine, sasa Mungu anakuletea mke wako we unazima simu 😅😅
Huwezi ona tatizo mpaka yakupate...
 
Khabarini wana jukwaa.

Mwaka 2021 nilikutana na dada mmoja mzuri sana, mrembo, mwenye kuvutia na mpole sana ambaye mwanaume yeyote mwenye akili timamu lazima tu angempenda. Basi nikafanya mchakato nikapata mawasiliano yake. Baada ya kuwasiliana na kumueleza shida yangu hakuwa na hiyana hivyo tukaingia katika mahusiano japo alinambia kuwa yeye ni mke wa mtu na ana Watoto wawili.

Kusema kweli tulipendana, mpaka sasa nampenda sana. Mme wake ni mtu wa mishemishe, mara nyingi hayupo. Hivyo nilikuwa naenda usiku kulala kwake na siku nisipoenda basi nilikuwa nampigia simu huyo mpenzi wangu tunazungumza hadi usiku wa manane. Au chatting kwa WhatsApp au sms za kawaida. Japo tulifanya kwa siri sana na mtu asingeweza kugundua, hata rafiki zangu wa karibu hawakujua na rafiki zake pia hawakujua lolote.

Penzi letu lilinoga mno, ilifikia hatua nikawa namiliki CREDIT CARD ya mme wake, na haikuwa issue kufanya miamala midogo midogo. (sio kwamba nilikuwa nalelewa sema tu alinipenda na kuniamini kiufupi tunapendana) pia nilimpenda mno mtoto wake mdogo, nilikuwa nampelekea vizawadi zawadi nikienda kulala, nacheza nako in short ni kacheshi mno kale katoto na kalinipenda pia.

Wakuu, hakuna marefu yasiyo na ncha, hatimaye mwenyemke akajua kwamba mke wake anachepuka, (hapo ndipo chanzo cha tatizo langu) akajaribu kutafuta ajue anachepuka na nani, akatafuta mpaka akapata namba yangu, mke wake akanambia kuhusu hili hivyo tukakubaliana tusitumiane sms na atakuwa ananitafuta yeye. Na mimi niliamua kuchukua extra precaution ikiwa ni Pamoja na kutopokea namba ngeni, pia mke wake alikuwa akinipigia nikipokea nasubiri aanze yeye kuongea ndo na mimi niongee. Baada ya jamaa kuona sipokei namba ngeni wala kujibu sms za namba ngeni aliamua kutafuta jina nililosajiria laini, nashukuru mungu laini yangu hiyo nilisajiri kwa jina la mtu mwingine na mtu huyo alikuwa mkoani hivyo asingeweza kunifahamu.

Baada ya harakati za kunitafuta kugonga mwamba, jamaa aliamua Kwenda mkoani kuendelea na mishe zake. Mimi na mpenzi wangu tukarudisha mapenzi na tukaendelea kuchati na kupeana mambo kama kawaida. Siku ya jumamosi mwezi wa nne tarehe 13 jamaa alirudi, na mke wake alinijuza juu ya ujio wake. Usiku mida ya saa 4 kuna message moja illingia WhatsApp kutoka namba ngeni nanukuu

“NIMEAMUA KUKUACHIA HUYO MWANAMKE, KESHO ATAKUJA MUANZE NAE MAISHA, MIMI NTABAKI NA WANANGU. ASANTE SANA MWANAUME MWENZANGU”

Ujumbe huu ulinishitua sana na ukizingatia ulikuwa umeeandikwa kwa maandishi makubwa kuonesha msisitizo, kusema kweli niliamua kuhama ghetto nikaenda logde kulala ili kulinda usalama wangu maana nilihisi kama naweza patwa na jambo baya. Pia simu nilizima ili isije kuwa tracked nikapatikana kiboya. Usiku sikupata usingizi hata kidogo yaani hata kufumba tu macho hakuna. (acheni jamani watu tunapitia shida sana hapa Tanzania duh) kuna mda natamani hata niwe mkimbizi Afghanistan kuliko kuishi hapa Bongo.

Kuna jambo moja ambalo mke wake hakunambia na alinambia ikiwa ni too late. Kumbe jamaa alimpa zawadi ya simu kabla hajarudi mkoani kwenye mishe zake, simu hiyo alikuwa ameihack achilia mbali normal sms and calls, hata chatting za WhatsApp alikuwa anaziona na kuzisoma. Jambo hili lilinishitua sana maana nilijua atakuwa amenasa pia picture zangu tunazotumiana na mkewe hivyo kudakwa ni suala la muda tu.

Kwa ufupi ni kwamba.

Jana Asubuhi na mapema nilihama huo mtaa, nikaenda mtaa mwingine mbali kabisaa maana nilihisi jamaa anaweza niletea huyo mke wake hadi kwangu. hivyo asubuhi na mapema niliita Kirikuu ikabeba vitu vyangu nikasepa. Leo saa 4 usiku nikapokea simu ya huyu mwanamke (mpenzi wangu) akanambia kwamba

baba jay (code) amekuja na mwanamke mwingine, mimi amenifukuza amekatalia watoto wake nimekuja hapo kwako wamesema umehama, kwanini umehama bila kunambia? Uko wapi nahitaji tuzungumze.

Ujumbe huu umefanya nikatetemeka kuanzia unyayo mpaka utosi, sikutarajia jambo kama hili, huyu mwanamke anasema anataka aje tuishi, pia nimsaidie afungue shauri mahakamani ili apewe talaka, mgawo wa mali na Watoto pia. Yaani niko njia panda nawaza nimuelekeze nilipo? Dah! Hata sielewi… na mimi sina mpango wa kuoa saa hizi. Yaani kimsingi sitaki kabisaa mambo ya kuoa iwe leo au kesho. Hata nikitaka kuoa siwezi oa single mother, nyumbani watanielewaje? Wakiskia story kuhusu huyu mpenzi wangu je itakuwaje? Duh.

Mambo ni mengi sema siwezi Andika yote ntapoteza muda wenu bure.

Ndugu zangu naombeni Mnishauri nina shida sana. Yaani dunia imekuwa chungu sana kwangu, naishi kwa kujificha kama mnyama duh! Nimechoka na maisha ya utumwa. (better die free than living as a slave)

Endelea 👇 👇

Msaada: Mke wa mtu anataka kuhamia Kwangu
Kama jamaa kaenda na mwanamke mwingine kwake,basi beba huyo mwanamke wake,hawezi kufanya lolote,asingeenda na mwanamke mwingine angeishia kumfukuza tu basi ningekwambia usimchukue kabisa ninhatari,lakini huyo beba na mkakae mbali ikiwezekana mkoani
 
Mungu akusamehe kwa kuhamasisha ushoga...
Basi nakuombea wakufirimbe !!..wakupake kirainishi kwa kuharibu familia ya watu….
Ao watoto wakianza kuteseka na kuranda randa kisa niww uliharibu hiyo familia
 
Kama jamaa kaenda na mwanamke mwingine kwake,basi beba huyo mwanamke wake,hawezi kufanya lolote,asingeenda na mwanamke mwingine angeishia kumfukuza tu basi ningekwambia usimchukue kabisa ninhatari,lakini huyo beba na mkakae mbali ikiwezekana mkoani
Nampenda sana, ila sintaweza. Nashukuru Mungu Wamesameheana. Inshallah
 
Tatizo huna ustaarabu mdogo Angu, hivi unadhani nilifanya kwa kupenda? Maisha ni fumbo hujui kesho yako...
Leo kwangu kesho kwako.
Kwaiyo ilikua paap ukaangukia kwene k ya mke wa mtu.
Ukashtuka ukakuta n mke wa mtu ukasema ebu uendelee
Ukachukua na kadi ukaenda kutoa hela zake…
Kifupi we n marioo unapenda kula hela za wanaume wenzio
 
Mi sina muda !! hao ulozoea kuwalia wake watalala na ww
Na lengo LA kuandika hii thread ni kuomba msaada (ushauri) na sio matusi...
Jaribu kuelewa hali ya mwanaume mwenzako kila mtu hufanya kosa na anahaki ya kusamehewa...
Naamini umenielewa.
 
Kwaiyo ilikua paap ukaangukia kwene k ya mke wa mtu.
Ukashtuka ukakuta n mke wa mtu ukasema ebu uendelee
Ukachukua na kadi ukaenda kutoa hela zake…
Kifupi we n marioo unapenda kula hela za wanaume wenzio
Kwahyo umekuja kunitukana?
 
Na lengo LA kuandika hii thread ni kuomba msaada (ushauri) na sio matusi...
Jaribu kuelewa hali ya mwanaume mwenzako kila mtu hufanya kosa na anahaki ya kusamehewa...
Naamini umenielewa.
😂😂😂😂Yaan huyo uliyemkosea hujamuomba msamaha unakuja mtandaoni??
au uliona ID yake huku!!
We mpigie simu au tuma watu waende hapa umeleta usikie watu wanamtazamk gan
 
Back
Top Bottom