Msaada: Mke wa mtu anataka kuhamia kwangu

Wake za watu wameponza wengi, unaenda kuongeza idadi yao.
Jiandae kisaikolojia.
 
Pole Sana , Ila hiyo ni hatua nzuri ya kujitafakari ili kuwa MTU bora.

Tatizo sio wewe na tatizo sio huyo mwanamke

Tatizo hapo lipo ktk kutojua maana ya useful na important.

Mke wa MTU - ni useful ana manufaa Ila sio muhimu , ni Kama gari na miguu yako , miguu ni important muhimu Ila gari lina manufaa useful.

Ushauri.

Njia ya kwanza nikulikubali tatizo na kuomba msamaha then mwambie ukweli huyo mwanamke kuwa hauwezi kumuoa.

Huyo mwanamke na wewe nyote mmetengeneza hatia (guilty) hivyo kuna Deni tayari mnadaiwa na njia ya kulilipa ni nyie kubadilika na kuwa watu wema.

Kuhusu kufatiliwa na kuuliwa n.k huyo mwanaume hatoendelea kukufatilia maana mke wake. Alikuwa useful na sio important alikuwa Ana manufaa Ila sio muhimu. that's why amekuwa replaced.

"You can't sacrifice someone else's life for ur life there's a karma debt has to be paid"

Tunaweza kuwasiliana , ili upate therapy na kujitoa ktk hatia na kuwa innocence - mnyongofu.
 
Kwa ushauri wangu. Huyo mwanamke achana nae ikiwezekana badilisha namba, naelewa hali unayopitia hata mimi yamewahi nikuta kuna jamaa alikuwa anaishi na mwanamke wake. Sema yeye alikuwa hajamuoa ila wamechukuana tu ni kama mke yaani, huyo mwanamke alizaa na huyo mwanaume watoto 2 nili date nae muda mrefu. Jamaa yake akagundua namega tunda lake akanipgia simu akaniambia nichague moja nimuache mkewe au aniletee home. Nilishtuka sana yule mwanamke wake alikuwa king'ang'anizi bahati nzuri, nilipata mishe mkoa mwingine nikahama
 
Hapa nimesoma comments nmekuja na moja kubwa" mwanamke mjinga huibomoa ndoa yake kwa mikono yake hata jamii yake humuona yeye ni mwenye hatia , mwanaume mjinga kuwa na michepuko ni urijali , hata rafiki zake humsifia.."
 
Kwanza huyo mume wake yupo smart kuliko wewe. Pili, huyo mwanamke kaachwa kimtego, watu wa Ball tunasema mwamba anavizia counter attack. Anajua huyo mwanamke ndiyo atakayekuingiza kwenye 18 zake. Ngoja nikupe akili kidogo...

Logically, haiwezekani Mwanamke mwenye stara ya kuwa mke wa mtu akubali kupelekwa kwenye boma ambayo tayari kuna mke mwingine halafu aendelee kukaa hapo baada ya kuona mwenzake anafukuzwa kama mbwa na watoto ananyang'anywa. So it means huyo mwanamke aliyeenda naye hapo kwake sio mke, bali ni mchongo wa kukamilisha plan yake ya kukudaka. Angekua ana mpango wa kumuacha wala asingejaribu kukutafuta toka mwanzo, it means alikua anataka akuchimbe beat umuachie mke wake, sema wewe ukajifanya mjanja. Kwahiyo hisia zako hazikudanganyi. Kuna namna anataka kufanya revenge!

Ushauri, usije ukajaribu kumchukua huyo mwanamke ukaishi naye. Itapendeza kama utabadilisha line na simu as soon as possible na usiwasiliane na huyo mwanamke tena. Ikiwezekana, hama tena hapo ulipohamia sasahivi.

Sema maamuzi yoyote utakayochukua, bado yatakua mafanikio kwenye mpango wa mume wake because it's either amrudie mke wake au akupate wewe. Ila bado nakushauri tena, chukua maamuzi ya kupotea kabisa and never come back to that Family again.

Na uache upumbavu! Mla vya wenzie na vyake huliwa!

Japo story yako imekaa kimchongo, either ni uongo au umeiokota kijiweni. Victim wa kweli wa tatizo asingeandika kama ulivyoandika wewe!
 
Huyo mwanamke na wewe nyote mmetengeneza hatia (guilty) hivyo kuna Deni tayari mnadaiwa na njia ya kulilipa ni nyie kubadilika na kuwa watu wema.

Kuhusu kufatiliwa na kuuliwa n.k huyo mwanaume hatoendelea kukufatilia maana mke wake. Alikuwa useful na sio important alikuwa Ana manufaa Ila sio muhimu. that's why amekuwa replaced.

"You can't sacrifice someone else's life for ur life there's a karma debt has to be paid"
Tunaweza kuwasiliana , ili upate therapy na kujitoa ktk hatia na kuwa innocence - mnyongofu.
Nimependa hii quote.
=

Life Choices and Karma: How They Shape Our Destiny

In the grand theatre of life, every choice we make sets a chain of events into motion. This is not just a principle of physics, but a universal law of Karma. Our actions, particularly those affecting others, send ripples through the cosmos, inevitably circling back to us.

Choosing to sacrifice another’s well-being for personal gain creates a karmic debt, a negative balance in the cosmic ledger that demands repayment. This debt can manifest in myriad ways - guilt, misfortune, or even attracting harm akin to what we inflicted.

The universe, in its intricate dance of balance, constantly seeks equilibrium. Thus, the choices we make matter. Opting for compassion, fairness, and empathy becomes not just a moral imperative, but a path to a harmonious existence.

By understanding the interconnectedness of our actions and their consequences, we can navigate life with a heightened sense of responsibility. This awareness allows us to minimize our karmic debt, fostering a more positive, harmonious existence, and truly comprehend how our life choices and Karma shape our destiny.
 
Khabarini wana jukwaa.

Mwaka 2021 nilikutana na dada mmoja mzuri sana, mrembo, mwenye kuvutia na mpole sana ambaye mwanaume yeyote mwenye akili timamu lazima tu angempenda. Basi nikafanya mchakato nikapata mawasiliano yake. Baada ya kuwasiliana na kumueleza shida yangu hakuwa na hiyana hivyo tukaingia katika mahusiano japo alinambia kuwa yeye ni mke wa mtu na ana Watoto wawili.

Kusema kweli tulipendana, mpaka sasa nampenda sana. Mme wake ni mtu wa mishemishe, mara nyingi hayupo. Hivyo nilikuwa naenda usiku kulala kwake na siku nisipoenda basi nilikuwa nampigia simu huyo mpenzi wangu tunazungumza hadi usiku wa manane. Au chatting kwa WhatsApp au sms za kawaida. Japo tulifanya kwa siri sana na mtu asingeweza kugundua, hata rafiki zangu wa karibu hawakujua na rafiki zake pia hawakujua lolote.

Penzi letu lilinoga mno, ilifikia hatua nikawa namiliki CREDIT CARD ya mme wake, na haikuwa issue kufanya miamala midogo midogo. (sio kwamba nilikuwa nalelewa sema tu alinipenda na kuniamini kiufupi tunapendana) pia nilimpenda mno mtoto wake mdogo, nilikuwa nampelekea vizawadi zawadi nikienda kulala, nacheza nako in short ni kacheshi mno kale katoto na kalinipenda pia.

Wakuu, hakuna marefu yasiyo na ncha, hatimaye mwenyemke akajua kwamba mke wake anachepuka, (hapo ndipo chanzo cha tatizo langu) akajaribu kutafuta ajue anachepuka na nani, akatafuta mpaka akapata namba yangu, mke wake akanambia kuhusu hili hivyo tukakubaliana tusitumiane sms na atakuwa ananitafuta yeye. Na mimi niliamua kuchukua extra precaution ikiwa ni Pamoja na kutopokea namba ngeni, pia mke wake alikuwa akinipigia nikipokea nasubiri aanze yeye kuongea ndo na mimi niongee. Baada ya jamaa kuona sipokei namba ngeni wala kujibu sms za namba ngeni aliamua kutafuta jina nililosajiria laini, nashukuru mungu laini yangu hiyo nilisajiri kwa jina la mtu mwingine na mtu huyo alikuwa mkoani hivyo asingeweza kunifahamu.

Baada ya harakati za kunitafuta kugonga mwamba, jamaa aliamua Kwenda mkoani kuendelea na mishe zake. Mimi na mpenzi wangu tukarudisha mapenzi na tukaendelea kuchati na kupeana mambo kama kawaida. Siku ya jumamosi mwezi wa nne tarehe 13 jamaa alirudi, na mke wake alinijuza juu ya ujio wake. Usiku mida ya saa 4 kuna message moja illingia WhatsApp kutoka namba ngeni nanukuu

“NIMEAMUA KUKUACHIA HUYO MWANAMKE, KESHO ATAKUJA MUANZE NAE MAISHA, MIMI NTABAKI NA WANANGU. ASANTE SANA MWANAUME MWENZANGU”

Ujumbe huu ulinishitua sana na ukizingatia ulikuwa umeeandikwa kwa maandishi makubwa kuonesha msisitizo, kusema kweli niliamua kuhama ghetto nikaenda logde kulala ili kulinda usalama wangu maana nilihisi kama naweza patwa na jambo baya. Pia simu nilizima ili isije kuwa tracked nikapatikana kiboya. Usiku sikupata usingizi hata kidogo yaani hata kufumba tu macho hakuna. (acheni jamani watu tunapitia shida sana hapa Tanzania duh) kuna mda natamani hata niwe mkimbizi Afghanistan kuliko kuishi hapa Bongo.

Kuna jambo moja ambalo mke wake hakunambia na alinambia ikiwa ni too late. Kumbe jamaa alimpa zawadi ya simu kabla hajarudi mkoani kwenye mishe zake, simu hiyo alikuwa ameihack achilia mbali normal sms and calls, hata chatting za WhatsApp alikuwa anaziona na kuzisoma. Jambo hili lilinishitua sana maana nilijua atakuwa amenasa pia picture zangu tunazotumiana na mkewe hivyo kudakwa ni suala la muda tu.

Kwa ufupi ni kwamba.

Jana Asubuhi na mapema nilihama huo mtaa, nikaenda mtaa mwingine mbali kabisaa maana nilihisi jamaa anaweza niletea huyo mke wake hadi kwangu. hivyo asubuhi na mapema niliita Kirikuu ikabeba vitu vyangu nikasepa. Leo saa 4 usiku nikapokea simu ya huyu mwanamke (mpenzi wangu) akanambia kwamba

baba jay (code) amekuja na mwanamke mwingine, mimi amenifukuza amekatalia watoto wake nimekuja hapo kwako wamesema umehama, kwanini umehama bila kunambia? Uko wapi nahitaji tuzungumze.

Ujumbe huu umefanya nikatetemeka kuanzia unyayo mpaka utosi, sikutarajia jambo kama hili, huyu mwanamke anasema anataka aje tuishi, pia nimsaidie afungue shauri mahakamani ili apewe talaka, mgawo wa mali na Watoto pia. Yaani niko njia panda nawaza nimuelekeze nilipo? Dah! Hata sielewi… na mimi sina mpango wa kuoa saa hizi. Yaani kimsingi sitaki kabisaa mambo ya kuoa iwe leo au kesho. Hata nikitaka kuoa siwezi oa single mother, nyumbani watanielewaje? Wakiskia story kuhusu huyu mpenzi wangu je itakuwaje? Duh.

Mambo ni mengi sema siwezi Andika yote ntapoteza muda wenu bure.

Ndugu zangu naombeni Mnishauri nina shida sana. Yaani dunia imekuwa chungu sana kwangu, naishi kwa kujificha kama mnyama duh! Nimechoka na maisha ya utumwa. (better die free than living as a slave)
Vijana mtapakwa mafuta ivi ivi mkijiona.
 
Unaharibu ndoa ya watu halafu una omba ushauri? Uko serious kweli? Umesambaratisha familia ya mwanaume mwenzio you deserve lolote litakalo kupata
 
umerudisha card yake kwanza?
anyway muoshwa huoshwa ,ukila vya wenzio nawe utaliwa ... relax subiri kuliwa kiboga hapo mzee cha muhimu kisafishe kwaajili ya jombiii
Kadi niliirudisha jumatano kaka ya tarehe 18
 
Attachments

  • Screenshot_20240421-004642~2.png
    Screenshot_20240421-004642~2.png
    278.8 KB · Views: 12
Kwanza huyo mume wake yupo smart kuliko wewe. Pili, huyo mwanamke kaachwa kimtego, watu wa Ball tunasema mwamba anavizia counter attack. Anajua huyo mwanamke ndiyo atakayekuingiza kwenye 18 zake. Ngoja nikupe akili kidogo...

Logically, haiwezekani Mwanamke mwenye stara ya kuwa mke wa mtu akubali kupelekwa kwenye boma ambayo tayari kuna mke mwingine halafu aendelee kukaa hapo baada ya kuona mwenzake anafukuzwa kama mbwa na watoto ananyang'anywa. So it means huyo mwanamke aliyeenda naye hapo kwake sio mke, bali ni mchongo wa kukamilisha plan yake ya kukudaka. Angekua ana mpango wa kumuacha wala asingejaribu kukutafuta toka mwanzo, it means alikua anataka akuchimbe beat umuachie mke wake, sema wewe ukajifanya mjanja. Kwahiyo hisia zako hazikudanganyi. Kuna namna anataka kufanya revenge!

Ushauri, usije ukajaribu kumchukua huyo mwanamke ukaishi naye. Itapendeza kama utabadilisha line na simu as soon as possible na usiwasiliane na huyo mwanamke tena. Ikiwezekana, hama tena hapo ulipohamia sasahivi.

Sema maamuzi yoyote utakayochukua, bado yatakua mafanikio kwenye mpango wa mume wake because it's either amrudie mke wake au akupate wewe. Ila bado nakushauri tena, chukua maamuzi ya kupotea kabisa and never come back to that Family again.

Na uache upumbavu! Mla vya wenzie na vyake huliwa!

Japo story yako imekaa kimchongo, either ni uongo au umeiokota kijiweni. Victim wa kweli wa tatizo asingeandika kama ulivyoandika wewe!
Asante sana mkuu. Shukhrani sana kwa ushauri kaka, napitia kipindi kigumu sana.... Naamini ntavuka. Inshallah.
 
Kwa ushauri wangu. Huyo mwanamke achana nae ikiwezekana badilisha namba, naelewa hali unayopitia hata mimi yamewahi nikuta kuna jamaa alikuwa anaishi na mwanamke wake. Sema yeye alikuwa hajamuoa ila wamechukuana tu ni kama mke yaani, huyo mwanamke alizaa na huyo mwanaume watoto 2 nili date nae muda mrefu. Jamaa yake akagundua namega tunda lake akanipgia simu akaniambia nichague moja nimuache mkewe au aniletee home. Nilishtuka sana yule mwanamke wake alikuwa king'ang'anizi bahati nzuri, nilipata mishe mkoa mwingine nikahama
Asante kwa muongozo mkuu... Mungu akutunze... Asante sana
 
Back
Top Bottom