Msaada: Mke wa mtu anataka kuhamia kwangu

Msaada: Mke wa mtu anataka kuhamia kwangu

Duuuuh kama sio chai.

Jamaa umezingua Sana.

Nikuulize swali.
Hivi wakielewana si mtaendeleza mahusiano au utamuacha?

Sio vizuri kutembea na mke wa mtu, hujui huyo jamaa kapitia wapi na mkewe.

Pia ameamua kukuachia wewe, na ujue hili ipo siku na wewe utagongewa nje, sababu hiyo ndio tabia yake huyo mwanamke na wewe pia utagonga nje hivyo utamuumiza huyo mwanamke. ( Na huyo mwanamke atajuta)

Mapenzi matamu Kwa sababu humtunzi wewe, Sasa Anza kumtumza uone, ili uone kama mapenzi yana raha zile mlizokuwa mkidanganyana.

Na kumbuka ukianza kuishi na huyo mwanamke kumbuka ameishazaa na jamaa, na Wazazi huwa hawaachani.

Mbeleni mwanamke atakuchoka jamaa atajilia mkewe kiulani tu Sasa sijui utajisikiaje.

Mwisho.
Usijaribu kuishi na huyo mwanamke. Sababu ni kosa juu ya kosa "kumbuka kisa cha Daudi na Mke wa Jenerali wake."

Mtakuwa mnazini maisha yenu yote sababu mume wake bado yupo hai hajafa.

Omba msamaha Kwa Jamaa, sio lazima ukutane nae. Wala usimshawishi amrudie mkewe ( Hilo ataamua mwenyewe) Sababu anaweza hisi unamlazimisha amrudie halafu uendelee kujilia maana amekuachia umeshindwa kujilia Kwa uhuru.

Omba msamaha Kwa huyo mwanamke Kwa kumuharibia ndoa yake.

Pia huyo mwanamke akubali tu amevunja ndoa yake Kwa mikono yake mwenyewe.

Omba msamaha Kwa Mungu.

Endelea na maisha yako.
Akhsante sana mkuu kwa ushauri wako. Mungu akutunze...
 
Ko



Nakushauri ndugu andika wosia kwa kidogo ulichonacho,
Tumia muda mwingi kuomba mungu akupokee licha ya hayo yote uliyoyafanya.
Ogopa sana siku za witiri(zisozagawantika kwa mbili) yaan jumatatu, jumatano, ijumaa na jumamosi.
Ujinga wako unakupeleka mwisho, hasara ilioje mke anabaki na maisha yake.
Kaka. Naamini hili pia litapita. Mungu atanisamamia. Inshallah
Akhsante kwa ushauri wako.
 
jiaandae kupakwa mafuta hadi utumbo utoke nje iyo kesi haijaisha kirahisi ivo jamaa anakulia timing tu na utanasa tu maan picha zako anazo
jipange ndugu
 
Hapa hamna haja ya wataalam kuja ... maelezo yako unasema mlipendana wenyewe mpaka unatumia ATM CARD ya mwanaume mwezako unajiona kidume...mzee kaa tuu ña huyo mwanamke maana hujui mwanamke ataamua nini baada ya wewe kukataa kuishi nae.acha undezi
 
Hapa hamna haja ya wataalam kuja ... maelezo yako unasema mlipendana wenyewe mpaka unatumia ATM CARD ya mwanaume mwezako unajiona kidume...mzee kaa tuu ña huyo mwanamke maana hujui mwanamke ataamua nini baada ya wewe kukataa kuishi nae.acha undezi
Mmmhhhh! Hapa ndo mnaponichanganya...
 
Khabarini wana jukwaa.

Mwaka 2021 nilikutana na dada mmoja mzuri sana, mrembo, mwenye kuvutia na mpole sana ambaye mwanaume yeyote mwenye akili timamu lazima tu angempenda. Basi nikafanya mchakato nikapata mawasiliano yake. Baada ya kuwasiliana na kumueleza shida yangu hakuwa na hiyana hivyo tukaingia katika mahusiano japo alinambia kuwa yeye ni mke wa mtu na ana Watoto wawili.

Kusema kweli tulipendana, mpaka sasa nampenda sana. Mme wake ni mtu wa mishemishe, mara nyingi hayupo. Hivyo nilikuwa naenda usiku kulala kwake na siku nisipoenda basi nilikuwa nampigia simu huyo mpenzi wangu tunazungumza hadi usiku wa manane. Au chatting kwa WhatsApp au sms za kawaida. Japo tulifanya kwa siri sana na mtu asingeweza kugundua, hata rafiki zangu wa karibu hawakujua na rafiki zake pia hawakujua lolote.

Penzi letu lilinoga mno, ilifikia hatua nikawa namiliki CREDIT CARD ya mme wake, na haikuwa issue kufanya miamala midogo midogo. (sio kwamba nilikuwa nalelewa sema tu alinipenda na kuniamini kiufupi tunapendana) pia nilimpenda mno mtoto wake mdogo, nilikuwa nampelekea vizawadi zawadi nikienda kulala, nacheza nako in short ni kacheshi mno kale katoto na kalinipenda pia.

Wakuu, hakuna marefu yasiyo na ncha, hatimaye mwenyemke akajua kwamba mke wake anachepuka, (hapo ndipo chanzo cha tatizo langu) akajaribu kutafuta ajue anachepuka na nani, akatafuta mpaka akapata namba yangu, mke wake akanambia kuhusu hili hivyo tukakubaliana tusitumiane sms na atakuwa ananitafuta yeye. Na mimi niliamua kuchukua extra precaution ikiwa ni Pamoja na kutopokea namba ngeni, pia mke wake alikuwa akinipigia nikipokea nasubiri aanze yeye kuongea ndo na mimi niongee. Baada ya jamaa kuona sipokei namba ngeni wala kujibu sms za namba ngeni aliamua kutafuta jina nililosajiria laini, nashukuru mungu laini yangu hiyo nilisajiri kwa jina la mtu mwingine na mtu huyo alikuwa mkoani hivyo asingeweza kunifahamu.

Baada ya harakati za kunitafuta kugonga mwamba, jamaa aliamua Kwenda mkoani kuendelea na mishe zake. Mimi na mpenzi wangu tukarudisha mapenzi na tukaendelea kuchati na kupeana mambo kama kawaida. Siku ya jumamosi mwezi wa nne tarehe 13 jamaa alirudi, na mke wake alinijuza juu ya ujio wake. Usiku mida ya saa 4 kuna message moja illingia WhatsApp kutoka namba ngeni nanukuu

“NIMEAMUA KUKUACHIA HUYO MWANAMKE, KESHO ATAKUJA MUANZE NAE MAISHA, MIMI NTABAKI NA WANANGU. ASANTE SANA MWANAUME MWENZANGU”

Ujumbe huu ulinishitua sana na ukizingatia ulikuwa umeeandikwa kwa maandishi makubwa kuonesha msisitizo, kusema kweli niliamua kuhama ghetto nikaenda logde kulala ili kulinda usalama wangu maana nilihisi kama naweza patwa na jambo baya. Pia simu nilizima ili isije kuwa tracked nikapatikana kiboya. Usiku sikupata usingizi hata kidogo yaani hata kufumba tu macho hakuna. (acheni jamani watu tunapitia shida sana hapa Tanzania duh) kuna mda natamani hata niwe mkimbizi Afghanistan kuliko kuishi hapa Bongo.

Kuna jambo moja ambalo mke wake hakunambia na alinambia ikiwa ni too late. Kumbe jamaa alimpa zawadi ya simu kabla hajarudi mkoani kwenye mishe zake, simu hiyo alikuwa ameihack achilia mbali normal sms and calls, hata chatting za WhatsApp alikuwa anaziona na kuzisoma. Jambo hili lilinishitua sana maana nilijua atakuwa amenasa pia picture zangu tunazotumiana na mkewe hivyo kudakwa ni suala la muda tu.

Kwa ufupi ni kwamba.

Jana Asubuhi na mapema nilihama huo mtaa, nikaenda mtaa mwingine mbali kabisaa maana nilihisi jamaa anaweza niletea huyo mke wake hadi kwangu. hivyo asubuhi na mapema niliita Kirikuu ikabeba vitu vyangu nikasepa. Leo saa 4 usiku nikapokea simu ya huyu mwanamke (mpenzi wangu) akanambia kwamba

baba jay (code) amekuja na mwanamke mwingine, mimi amenifukuza amekatalia watoto wake nimekuja hapo kwako wamesema umehama, kwanini umehama bila kunambia? Uko wapi nahitaji tuzungumze.

Ujumbe huu umefanya nikatetemeka kuanzia unyayo mpaka utosi, sikutarajia jambo kama hili, huyu mwanamke anasema anataka aje tuishi, pia nimsaidie afungue shauri mahakamani ili apewe talaka, mgawo wa mali na Watoto pia. Yaani niko njia panda nawaza nimuelekeze nilipo? Dah! Hata sielewi… na mimi sina mpango wa kuoa saa hizi. Yaani kimsingi sitaki kabisaa mambo ya kuoa iwe leo au kesho. Hata nikitaka kuoa siwezi oa single mother, nyumbani watanielewaje? Wakiskia story kuhusu huyu mpenzi wangu je itakuwaje? Duh.

Mambo ni mengi sema siwezi Andika yote ntapoteza muda wenu bure.

Ndugu zangu naombeni Mnishauri nina shida sana. Yaani dunia imekuwa chungu sana kwangu, naishi kwa kujificha kama mnyama duh! Nimechoka na maisha ya utumwa. (better die free than living as a slave)

Endelea 👇 👇

Msaada: Mke wa mtu anataka kuhamia Kwangu
Kwakweli mwanamke mjinga amevuna alichopanda, japo hii ni chai mimi nimemkubali jamaa kwa kufanya maaumizi ya kiume, huyo Mwanamke hakuwa mke bali ni tapeli la mapenzi na ndio maana badala ya kutafuta suluhu ya ndoa yake amekimbilia kutafuta mali na watoto.
 
Ishi na huyo mwanamke, ukimuacha lolote linaweza kutokea kama sio kujitanguliza mbinguni.
Kuhusu usalama wako/wenu; hama mkoa.​
 
Kwakweli mwanamke mjinga amevuna alichopanda, japo hii ni chai mimi nimemkubali jamaa kwa kufanya maaumizi ya kiume, huyo Mwanamke hakuwa mke bali ni tapeli la mapenzi na ndio maana badala ya kutafuta suluhu ya ndoa yake amekimbilia kutafuta mali na watoto.
Usimdharau usiyemjua....
 
Mmmhhhh! Hapa ndo mnaponichanganya...
Sasa mkuu apo mm nimekuchanganya nini?..kwani muda wote mko kwenye mahusiano hukujua kua ni mke wa mtu na siku zote haya mambo hua mwisho wake sio mzuri...mm nishakwambia ishi na huyo manzi ila ukae kwa password mana haujui jamaa ake ni kweli kakuchia kiroho safi ama laaah
 
N
Sasa mkuu apo mm nimekuchanganya nini?..kwani muda wote mko kwenye mahusiano hukujua kua ni mke wa mtu na siku zote haya mambo hua mwisho wake sio mzuri...mm nishakwambia ishi na huyo manzi ila ukae kwa password mana haujui jamaa ake ni kweli kakuchia kiroho safi ama laaah
Ngoja ni settle kwanza... Akili yangu itulie
 
Ishi na huyo mwanamke, ukimuacha lolote linaweza kutokea kama sio kujitanguliza mbinguni.
Kuhusu usalama wako/wenu; hama mkoa.​
Mkoa nimehama, ntaishi nae kama nikijiridhisha beyond reasonable doubt kwamba wameachana.
 
Naamini atanisamehe tu kaka....
sio rahisi kukusamehe as long atabak na watoto so kila akiwaona anawaza kuna fala kamrubuni mama yao au akioa alafu yule mke amzingue bado atarud kwako kuwa wew ndo chanzo cha yote,bro just run and hide kwa usalama wako sababu jamaa atakuja kwako kwa nguvu,uchungu na hasira nyingi hata kama si leo,hivyo ndivo wanaume tulivyo!
 
sio rahisi kukusamehe as long atabak na watoto so kila akiwaona anawaza kuna fala kamrubuni mama yao au akioa alafu yule mke amzingue bado atarud kwako kuwa wew ndo chanzo cha yote,bro just run and hide kwa usalama wako sababu jamaa atakuja kwako kwa nguvu,uchungu na hasira nyingi hata kama si leo,hivyo ndivo wanaume tulivyo!
Sawasawa. Sasa which is which? Dah! Ngoja nifikirie vizuri nione. Naamini Mungu ataniongoza. Inshallah
 
Back
Top Bottom