Msaada: Mke wa mtu anataka kuhamia kwangu

Msaada: Mke wa mtu anataka kuhamia kwangu

Jitahidi uwe naye karibu, atakuwa anapitia kwenye wakati mgumu sana
Bro! Sio kwamba nakimbia majukumu... Sema nimemuachia mda kama anaweza patana na mme wake wapatane tu. Kama wasipo patana then I will be responsible but for the time being wacha wajaribu kusolve tuone.... That's all
 
Sawasawa. Sasa which is which? Dah! Ngoja nifikirie vizuri nione. Naamini Mungu ataniongoza. Inshallah
huyo mwanamke achana nae mazima....what if jamaa anafanya monitoring mwenendo wenu hata kama utahama mkoa?jua huyo manzi ana ndugu ambao atawasiliana nao hata kama mtakua mmejificha,mbaya kwenu jamaa ana access na hao ndug so lazma tu atajua mliko na siku isiyo na jina utalia kama ndama na hakuna atakae kuokoa!ACHANA NA MKE WA MTU!
 
Khabarini wana jukwaa.

Mwaka 2021 nilikutana na dada mmoja mzuri sana, mrembo, mwenye kuvutia na mpole sana ambaye mwanaume yeyote mwenye akili timamu lazima tu angempenda. Basi nikafanya mchakato nikapata mawasiliano yake. Baada ya kuwasiliana na kumueleza shida yangu hakuwa na hiyana hivyo tukaingia katika mahusiano japo alinambia kuwa yeye ni mke wa mtu na ana Watoto wawili.

Kusema kweli tulipendana, mpaka sasa nampenda sana. Mme wake ni mtu wa mishemishe, mara nyingi hayupo. Hivyo nilikuwa naenda usiku kulala kwake na siku nisipoenda basi nilikuwa nampigia simu huyo mpenzi wangu tunazungumza hadi usiku wa manane. Au chatting kwa WhatsApp au sms za kawaida. Japo tulifanya kwa siri sana na mtu asingeweza kugundua, hata rafiki zangu wa karibu hawakujua na rafiki zake pia hawakujua lolote.

Penzi letu lilinoga mno, ilifikia hatua nikawa namiliki CREDIT CARD ya mme wake, na haikuwa issue kufanya miamala midogo midogo. (sio kwamba nilikuwa nalelewa sema tu alinipenda na kuniamini kiufupi tunapendana) pia nilimpenda mno mtoto wake mdogo, nilikuwa nampelekea vizawadi zawadi nikienda kulala, nacheza nako in short ni kacheshi mno kale katoto na kalinipenda pia.

Wakuu, hakuna marefu yasiyo na ncha, hatimaye mwenyemke akajua kwamba mke wake anachepuka, (hapo ndipo chanzo cha tatizo langu) akajaribu kutafuta ajue anachepuka na nani, akatafuta mpaka akapata namba yangu, mke wake akanambia kuhusu hili hivyo tukakubaliana tusitumiane sms na atakuwa ananitafuta yeye. Na mimi niliamua kuchukua extra precaution ikiwa ni Pamoja na kutopokea namba ngeni, pia mke wake alikuwa akinipigia nikipokea nasubiri aanze yeye kuongea ndo na mimi niongee. Baada ya jamaa kuona sipokei namba ngeni wala kujibu sms za namba ngeni aliamua kutafuta jina nililosajiria laini, nashukuru mungu laini yangu hiyo nilisajiri kwa jina la mtu mwingine na mtu huyo alikuwa mkoani hivyo asingeweza kunifahamu.

Baada ya harakati za kunitafuta kugonga mwamba, jamaa aliamua Kwenda mkoani kuendelea na mishe zake. Mimi na mpenzi wangu tukarudisha mapenzi na tukaendelea kuchati na kupeana mambo kama kawaida. Siku ya jumamosi mwezi wa nne tarehe 13 jamaa alirudi, na mke wake alinijuza juu ya ujio wake. Usiku mida ya saa 4 kuna message moja illingia WhatsApp kutoka namba ngeni nanukuu

“NIMEAMUA KUKUACHIA HUYO MWANAMKE, KESHO ATAKUJA MUANZE NAE MAISHA, MIMI NTABAKI NA WANANGU. ASANTE SANA MWANAUME MWENZANGU”

Ujumbe huu ulinishitua sana na ukizingatia ulikuwa umeeandikwa kwa maandishi makubwa kuonesha msisitizo, kusema kweli niliamua kuhama ghetto nikaenda logde kulala ili kulinda usalama wangu maana nilihisi kama naweza patwa na jambo baya. Pia simu nilizima ili isije kuwa tracked nikapatikana kiboya. Usiku sikupata usingizi hata kidogo yaani hata kufumba tu macho hakuna. (acheni jamani watu tunapitia shida sana hapa Tanzania duh) kuna mda natamani hata niwe mkimbizi Afghanistan kuliko kuishi hapa Bongo.

Kuna jambo moja ambalo mke wake hakunambia na alinambia ikiwa ni too late. Kumbe jamaa alimpa zawadi ya simu kabla hajarudi mkoani kwenye mishe zake, simu hiyo alikuwa ameihack achilia mbali normal sms and calls, hata chatting za WhatsApp alikuwa anaziona na kuzisoma. Jambo hili lilinishitua sana maana nilijua atakuwa amenasa pia picture zangu tunazotumiana na mkewe hivyo kudakwa ni suala la muda tu.

Kwa ufupi ni kwamba.

Jana Asubuhi na mapema nilihama huo mtaa, nikaenda mtaa mwingine mbali kabisaa maana nilihisi jamaa anaweza niletea huyo mke wake hadi kwangu. hivyo asubuhi na mapema niliita Kirikuu ikabeba vitu vyangu nikasepa. Leo saa 4 usiku nikapokea simu ya huyu mwanamke (mpenzi wangu) akanambia kwamba

baba jay (code) amekuja na mwanamke mwingine, mimi amenifukuza amekatalia watoto wake nimekuja hapo kwako wamesema umehama, kwanini umehama bila kunambia? Uko wapi nahitaji tuzungumze.

Ujumbe huu umefanya nikatetemeka kuanzia unyayo mpaka utosi, sikutarajia jambo kama hili, huyu mwanamke anasema anataka aje tuishi, pia nimsaidie afungue shauri mahakamani ili apewe talaka, mgawo wa mali na Watoto pia. Yaani niko njia panda nawaza nimuelekeze nilipo? Dah! Hata sielewi… na mimi sina mpango wa kuoa saa hizi. Yaani kimsingi sitaki kabisaa mambo ya kuoa iwe leo au kesho. Hata nikitaka kuoa siwezi oa single mother, nyumbani watanielewaje? Wakiskia story kuhusu huyu mpenzi wangu je itakuwaje? Duh.

Mambo ni mengi sema siwezi Andika yote ntapoteza muda wenu bure.

Ndugu zangu naombeni Mnishauri nina shida sana. Yaani dunia imekuwa chungu sana kwangu, naishi kwa kujificha kama mnyama duh! Nimechoka na maisha ya utumwa. (better die free than living as a slave)

Endelea 👇 👇

Msaada: Mke wa mtu anataka kuhamia Kwangu
Mkuu kitaalamu stori iwe fupi tu! Achana na Mke ya mtu! Wanawake wapo wengi! Manung'uniko ya mwanaume mwenzako sio kitu kizuri kabsa!

Kut 20:17
Usiitamani nyumba ya jirani yako, usimtamani mke wa jirani yako; wala mtumwa wake, wala mjakazi wake, wala ng’ombe wake, wala punda wake, wala cho chote alicho nacho jirani yako.

Kumbukumbu 5:21
Usitamani mke wa jirani yako. Usitamani nyumba ya jirani yako au shamba lake, mtumishi wake wa kiume au wa kike, ngʼombe au punda wake, wala kitu chochote cha jirani yako.”
 
Mkuu tumedumu kwenye mahusiano almost 4 years sasa. To be honest alikuwa kama Mke wangu tu. Four years nyingi sana... Na hapo kuna mambo sijataka kuyaweka hadharani.
Kama ameachwa mchukue uishi nae ana watoto wangapi
 
huyo mwanamke achana nae mazima....what if jamaa anafanya monitoring mwenendo wenu hata kama utahama mkoa?jua huyo manzi ana ndugu ambao atawasiliana nao hata kama mtakua mmejificha,mbaya kwenu jamaa ana access na hao ndug so lazma tu atajua mliko na siku isiyo na jina utalia kama ndama na hakuna atakae kuokoa!ACHANA NA MKE WA MTU!
Duh
 
Mkuu kitaalamu stori iwe fupi tu! Achana na Mke ya mtu! Wanawake wapo wengi! Manung'uniko ya mwanaume mwenzako sio kitu kizuri kabsa!

Kut 20:17
Usiitamani nyumba ya jirani yako, usimtamani mke wa jirani yako; wala mtumwa wake, wala mjakazi wake, wala ng’ombe wake, wala punda wake, wala cho chote alicho nacho jirani yako.

Kumbukumbu 5:21
Usitamani mke wa jirani yako. Usitamani nyumba ya jirani yako au shamba lake, mtumishi wake wa kiume au wa kike, ngʼombe au punda wake, wala kitu chochote cha jirani yako.”
Duh sawa mkuu
 
Pole mzee kwa mtihani saiv kaa utulize kichwa kwanza then utapata majibu sahihi
 
Kula mke wa mtu mwisho mara mbili tu.

Hii ni kwa mabazazi na wazinzi wote.

Usikate kuchomga mzinga litakupata.

Piga one, two , tembea. Acha Alie . Hata Kama ni mzuri kiasi gani!!

Ukitaka kujidai sharukh Khan!! ,Itakucost
 
Ila kuna watu mnazalau sana, mwanaume mwenzio unamfanyia usenge wa namna hivyo, kama ni mim nakutaftia mijuba, ikunyooshe, siku nyingne usirudie. Sasa hapo unataka tukupe mbinu za kukwepa kunywa uji uloukologa mwenyewe.
 
  • Mshahara wa dhambi ni mauti.
  • Maumivu ya kuchukuliwa mke ni makali kuliko ya kuchukuliwa mali.
  • Ukiiba vyaelea ujue vimeumbwa.
Ushauri! Kama vp tafuta wazee/ watu wa heshima waende kwa jamaa kukuombea nsamaha, ili uyabebe majukumu kwa Amani.
  • Mwenye mke akikubali, wakaachame mahakamani.
  • Huyo mkeo aseme wazi mbele ya mahakama kuwa mali alizochuma na jamaa ni mali ya watoto; YEYE ASICHUKUE CHOCHOTE!
 
Bro! Sio kwamba nakimbia majukumu... Sema nimemuachia mda kama anaweza patana na mme wake wapatane tu. Kama wasipo patana then I will be responsible but for the time being wacha wajaribu kusolve tuone.... That's all
Huyo dada hawezi kusamehewa na mume wake.
 
Issue sio kuoa ndugu yangu. Issue huyu ni Mke wa mtu. Namuoaje duh! Mi sijui hata kesho yangu... Inauma sana
Kwani wakati unamchakata hujui kama ni mke wa mtu? ila wee una roho ngumu kama paka, hadi unaenda kulala kwake? hadi watoto wake unawaletea zawadi? Kwa taarifa yako Hao watoto ndo informer wazuri kwa baba yao akirudi toka safarini. Vaa kiatu cha huyo mwanaume mwenzako mkeo afanyiwe hivyo unavyomfanyia ungemfanyia nini mwanaume anayetembea na mke wako? Kwa ufupi hujui tips za kudate mke wa mtu umejipeleka kichwa kichwa
 
Baada ya kumfanya mke wa mtu single mother ndo unakuja na point kwamba utaki kuoa single mother , kwani ulimkuta single mother????????

Wewe ni mwanaume take responsibility of the problems you caused , umeshaharibu ndoa ya watu na unakimbia we ni fala...

Ushauri wangu ukijiridhisha jamaa kweli amempiga chini mchukue mkaishi mkoa mwingine sababu wewe ndo chanzo cha matatizo yote hayo.....
 
Back
Top Bottom