Mke wangu alikuwa namna hiyo, alikuwa anakasirika ghafla afu baadae anapoa, nikaa nae kuongelea hali hiyo akasema hata yeye haipend ila inamtokea tu.nikawa namhimiza sana kusali kabla ya kulala nikawa nae karibu. Nikaacha kumkosoa hata akiharibu. Siku moja alinambia mambo flan mabaya niliyowahi kumfanyia. Aliongea sana akalia usiku kucha toka hapo hali hiyo ikaisha. Mkeo atakuwa amekaa na mengi moyoni mwake.