Msaada: Mke wangu mtarajiwa anawasiliana na ex wake, nifanyeje?

Duh kuna watu mna vipaji vya kupenda hata Shah Rukh Khan anasubiri. Ningekuwa karibu ningekusukumia konde moja takatifu sana la uso ungeziona nyota.

Nimelisoma gazeti lako lote sijaona hata sababu moja ya kukufanya umpende huyo MKE WA MTU. Nimetamani hata nione weakness moja kwenye gazeti lako at least nijifariji kuwa ni chai, lakini wapi!.

Kwa ujinga wako hapo andika wosia kabisa maana mwisho wako haupo mbali, aidha kwa kufumaniwa na huyo mumewe aliyetoa talaka moja akupelekee moto na akuue au ujiue kwa aibu, kufa kwa pressure/sukari/moyo kutokana na kupenda kizezeta usipopendeka, ama huyo mke wa jamaa (unayemuita mpenzi wako/mkeo mtarajiwa) akuue kwa kukuchoma na hicho kisu kilichopelekea akapewa talaka moja.
 
Mi sijasoma yote ila umejichanganya, hey brother, watoto wawili na alishaolewa, ebu kuwa serious, kipi kipya utafanya hapo, have some respect on yourself brother, wewe jitie mapenzi uone kitu kizito kinavyotua puani.
 
Kila jambo linasababu yake usione kuwa alikuwa anamnyanyasa kama unampenda mtathimini na jitathimini mnaakili timamu
 
Huu ndio ushauri bora wa mwaka 100%✅️✅️✅️✍️✍️✍️✍️✍️
 
Baada ya kuona na hataki kabisa mimi kuwaona watoto ambao ni kama wangu.
Kama watoto wako eeh?
Jitafutie matatizo yatakayofupisha uhai wako, huyo mke wa mtu unasumbukia nini na bado anaonesha dhahiri bado yupo sana kwa baba watoto wake? Hao hawatokaa waachane.

Mbona wanawake ni wengi sana mkuu.
 
Unaita watoto wa mwenzio watoto wako, unaita mwanamke ambae hata pete hujamvisha mke mtarajiwa.

Wewe jamaa ni yatima wa mpenzi. Hilo gubegube huliwezi.
Kuna wanawake wameumbiwa mateso sasa na wewe ukijifanya Shah Rukh Khan wa mapenzi utaishia matesoni.

Huyo hakupendi, achana nae.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…