Msaada mkopo wa ujenzi toka PSPF

Msaada mkopo wa ujenzi toka PSPF

kulyunga

JF-Expert Member
Joined
Oct 19, 2011
Posts
230
Reaction score
423
Habari zenu wakuu.. Kama bandiko langu lapo juu linavyojieleza nahitaji msaada jinsi ya kukamilisha upatikanaji wa mkopo tajwa manke nimehangaika sana na sasa ni kama naelekea kukata tamaa.

Niliomba mkopo tajwa mnamo mwezi december mwaka jana na baada ya kusumbuliwa sana na PSPF ngazi ya mkoa hatimae nikafanikiwa kukamilisha kila kilichohitajika kwa ajili ya mkopo huo ikiwa ni pamoja na hati ya kiwanja,hati za mishahara,cheti cha ndoa (kiwanja kina jina langu na la mke wangu) viapo vya mahakama vya kwangu na mke wangu kuhusu makubaliano ya kutumia kiwanja husika kuomba mkopo na nyaraka nyingine muhimu.

Baada ya nyaraka zangu kupokelewa mkoani nilisubiri kuanzia hiyo december hadi february mwishoni na hapo nilikuwa napiga simu kila baada ya muda kujua maendeleo lakini hakuna nililoambiwa hadi mwishoni mwa february nilipoletewa majibu kuwa inahitajika "spouce consent" toka kwa hakimu wa wilaya na sio kiapo kama nilivopeleka mimi (ndivo nilivyoelekezwa mwanzoni)

Tatizo linakuja hiyo spouse consent hakimu anasema ndo kile kile kiapo lakini niliandikiwa kingine na nilipokiwasilisha PSPF kimekataliwa tena. Naombeni msaada wenu kwa anayejua hii spouce consent inakuaje anisaidie jamani manake hali ni mbaya sasa..

Asanteni sana..
 
Hawana hela hao bwana unasumbuka tu...!wastahafu kuwalipa yenyewe shida itaweza kutoa mkopo wa nyumba
 
Hawana hela hao bwana unasumbuka tu...!wastahafu kuwalipa yenyewe shida itaweza kutoa mkopo wa nyumba

Najuta kujiunga na hawa wasanii mifuko mingine hawana longolongo kama hizi hasa LAPF.
 
Najuta kujiunga na hawa wasanii mifuko mingine hawana longolongo kama hizi hasa LAPF.


Sikushauri uendelee na hiyo mikopo utajuta!! riba pamoja na usumbufu... kwann usifanye serving au usikope personal loan?
 
Back
Top Bottom