Kila kitu kina mkataba kama anao mkataba unaomuambia umlipe hiyo pesa mpe...
Ila kiubinadamu kama amekulinda kwa miaka hiyo kiungwana mpe naye ajione mtu.... Pengine uhai wako Mwenyezi Mungu alilinda kupitia huyo jamaa...
Mimi siku hizi mali zangu nazikatia Bima tu nalipa once kwa Mwaka Gari linakaa nje tu mtaani likiibiwa naenda dai bima... Nyumba vile vile... nilipiga hesabu nikaona bima ndio muafaka... kama wezi wa kutoa roho siku ikifika imefika tu roho itatoka hata kukiwa na walinzi tena walinzi wetu ukipita wamelala hadi uwaamishe wewe... lol
Gari kuoshwa kwa siku ni 2,000 kwa mwaka kulindwa kwa usiku tu ni 2,000 kwa mwaka una siku 365 jumla ukilipa ni 730,000/= wakati nikilipa bima ni kama laki tatu hadi nne premium ya mwaka mzima bora nini! na walinzi wetu ukiibiwa hawakulipi... wanakuomba msamaha tu... tena unakuta ni kibabu haswa ukikipiga kibao kimoja hakiamki