Hongera mkuu na pole pia. Najua mliingoja sana hii mimba na sasa unakitarajia kije kikiwa kamili kabisa bila hata kope kuwa fupi kwa sababu ya jasho au joto la nchi.
Lakini, usihofu juu ya mama kupika, tena nakuambia ni vizuri awe anafanya mazoezi makali zaidi ya kupika. Nadhani umetokea kijijini, je hujawahi sikia wamama waliojifungulia shambani wakilima?? Mimi ni shahidi, nimewaona 2 waliojifungulia shambani wakilima tena mmoja alijifungua mapacha.