Mkuu Kubota nimezipenda sana makala zako kuhusu ujasiriamali. Mi nataka kuwekeza kwenye kilimo eidha kwa kufuga mbuzi/kuku na au kulima mbogamboga na matunda. Ili kufanikiwa katika hayo, maji ni sehemu muhimu sana. Nilifanya survey ya kuchimba kisima cha maji kwenye kishamba changu ili niyatumie kwa umwagiliaji nikaambiwa yapo chini umbali wa mita 150 na bei ikawa iko juu mno kama 14M hivi. Nimepania sana kufanya shughuli hizo za kilimo ili niachane na mambo ya kuajiriwa lakini tatizo ni hayo maji. Kama naweza kupata mchimbaji ambaye atanifanyia kazi hiyo kwa bei ya chini nitafurahi, uwezo wangu haufiki hata nusu ya hiyo bei niliyoisema hapo juu. Naombeni ushauri na mawazo pia wana JF.
Mkuu kama una eneo zuri na unaipenda project unganisha na wadau nguvu kazi ifanyike!!!
Ni bora kupata kidogo kuliko kukosa kabisa