Msaada, mtoto amegoma kunyonya

Msaada, mtoto amegoma kunyonya

Samboko

JF-Expert Member
Joined
Oct 30, 2011
Posts
5,420
Reaction score
7,788
Habari wana jf,

Mke wangu ana mtoto wa miezi mitatu 3, hii wiki ya tatu kagoma kunyonya kwa mama yake, akawa anamkamulia kwenye kikombe na kumnywesha lakini bado hataki kunywa, yaani anamnywesha kwa shida sana hadi amepungua sana tofauti na alivyokua awali, tumenunua maziwa ya unga nayo pia hataki kunywa,

Hatujui ana shida gani kwa kweli, na anaonekana yupo vizuri tuu, anacheka, anacheza ila shida hapo kwenye kula tuu, hospital amepelekwa lakini hana ugonjwa wowote
Naombeni msaada madaktari wa humu kama kuna mwenye kujua tatizo la mtoto au tiba yake ni nini aweze kula kama kawaida.
 
Watot wadogo wanasumbua sana,mwambie mkeo asichoke ampe hvyo hvyo mara nying awezavyo hata kama akinyw vijiko viwilo au vitatu badae kdgo ampe tena na tena,na pia asijali hyo n kawaida ya watoto wadogo wanabadlk kila uchwao, as long as hospt mmeambiw hana ttzo ,cha kukazana hapo n kumnyonyesha/kumpa kw njia yyte ile maziwa kila baad y muda mfup maana co mlaji
Hope nimeeleweka
Bye
 
Kila baada ya masaa 2 amnyonyeshe au amnyweshe hadi atakapo zoea Mama asichoke
 
Asante mkuu kwa ushauri, na nimekuelewa sana, ndivyo anavyofanya kwa sasa, ntamwambia azidi kumkazania zaidi
 
Kila baada ya masaa 2 amnyonyeshe au amnyweshe hadi atakapo zoea Mama asichoke
Sawa mkuu, ila alipozaliwa alkua ananyonya vizuri tuu,, ila kadri siku zinavyoenda anazidi kua msumbufu kula
 
Badilisha kipira cha kunyonyea na pia kwa miezi mitatu mpe uji au mchanganyie maziwa na cerelac kdg
 
Samboko mtafutieni multivitamin, Pia mama mtu akazane kumlisha na maji ya kunywa
 
Kwa mila za kiafrika, mtoto akizaliwa kama ana bibi na shangazi, inabidi wamfanyie tambiko kama ni sala au kama ni dua au kama ni tambiko za kienyeji. Chakula kipikwe kiliwe na ndugu na majirani. Mlifanya hivyo. Kuna koo ambazo lazima haya yafanyike hivyo jaribu hilo. Nina mifano miwili au mitatu ya sababu ya watoto kugoma na baada ya kuwapeleka kwa hao wakulu, basi watoto wananyonya.
 
Hata mimi nilishawahi kusikia hayo, lakini waliomtangulia hawakua na shida kama hii
 
Unajua kila mtoto na miungu yao na mizuka yao. Wengine sisi wa zamani bado tuna kale ka kuchanganya huku na huku.
 
Back
Top Bottom